CHANZO CHA UZIMA. *Sehemu ya kwanza*


Unapozungumzia uzima maana yake unazungumza juu ya mema au baraka.
Kama uzima ni mema au baraka basi mwanadamu wa leo anapasa kutambua na kuelewa ya kwamba ni njia gani aindee ili aweze kuufikia uzima.

Picha
Na mtumishi wa MUNGU Kabalama Masatu.

Maandiko katika Kumb.la Torati30:19-20 imeandikwa,
"Nazishuhudia mbingu na nchi juu yenu hivi leo,kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti,baraka na laana;basi chagua uzima,ili uwe hai wewe na uzao wako;kumpenda BWANA,Mungu wako,kuitii sauti yake,na kushikamana naye;kwani hiyo ndiyo uzima wako,na wingi wa siku zako;upate kukaa katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako,Ibrahimu,na Isaka,na Yakobo,kuwa atawapa".

Hawa wana wa Isreli walipewa "option" ya kuchagua,maana mbele yao tayari kulikuwa kuna hoja mbili yaani:-

(i).Hoja ya uzima(mema na baraka).


(ii).Hoja ya mauti (laana,mabaya na uharibifu).


Kwa hiyo jukumu lilikuwa kwenye maamuzi yao wenyewe.
Kuchagua uzima maana yake ni kuchagua kumpenda Bwana,kuitii sauti yake na kushikamana naye.


Kumbe "Chanzo cha uzima wa milele" ni kumpenda Bwana,Mungu wako,kutii sauti yake na kushikamana naye.
Oooooh,Alleluyah!


Mimi nalipenda sana jambo hili; kumpenda Bwana,Mungu wangu aliyeniumba,anayenipa uzima,afya na furaha.kuitii sauti yake;na kushikamana naye alafu malipo yangu ni kupewa uzima wa milele,kupewa mema,kupewa baraka.


Na Mungu anasema "amezishuhudia mbingu na nchi".Kumbe ni jambo la kweli kabisa wala siyo propaganda maana Mungu siyo mwanadamu hata aseme uongo.


Basi mimi nakushauri leo ndg,fanya uchaguzi sahihi,uchaguzi wako leo hapa duniani ndio unaohamua maisha yako baada ya kutoka duniani.Chagua uzima leo yaani Kumpenda Bwana,kumtii na kushikamana naye.


Utambue ya kwamba kama ukikosea kuchagua leo hii basi mauti iko mbele yako.Kwa nini uingie katika mauti wakati unao uwezo wa kufanya maamuzi sahihi leo hii?


ITAENDELEA...............
Mawasiliano ni:-
0753-305957;
0789-628226;
0717-624035.

Comments