Kazi imeanza kwa mtumishi wa Mungu ambaye amepata neema ya kudondoka
ndani ya Berlin. Hii ni changamoto kwetu sisi kuona mwimbaji kama huyu
anapata channel za ulaya. Ninaamini ukiwa chini ya miguu ya Baba yetu wa
mbinguni siku moja atakuweka mahali ambapo hukutegemea kufika.
Lakini
jitihada zako pia zinahitajika, juhudi zako za kutimiza ndoto zako
zikiwa kubwa ndipo milango ya mafanikio pia inafunguka. Tuzidi kuwa
mwaaminifu mbele za Mungu na tusichanganye ya duniani na ya mbinguni
kama shortcut ya mafanikio.
Muulize Mungu wako nini amekiweka ndani yako
kwa kazi yake ili uanze kukitumia sasa. David aliona uimbaji kwake ni
karama aliyopewa na Mungu na ndio maana akakaza buti na sasa anakaa na
ngozi nyeupe akichangia maoni yake. Jikubali na sema ninaweza.

David Robert
David Robert akiwa ametulia katika jopo la wazungu
Comments