DKT. BARNABAS MTOKAMBALI AWAASI WAUMINI NA WATANZANIA KUIOMBEA TANZANIA


Askofu mkuu wa Kanisa la Tanzania Asemblies of God TAG Dk Barnabas Mtokambali amewaasa waumini wa kanisa la TAG pamoja na watanzania kwa ujumla kuiombea nchi ya Tanzania kwa dhati kutokana na mapito inayoipitia kwanza ikiwa ni mchakato wa kupata Katiba Mpya,pili ni Uchaguzi mkuu unaonza na serikali za mitaa mwaka huu na mwakani madiwani,wabunge na hatimaye Rais na tatu ni kuhusu madini ambayo Mungu ametupa kwani yanatakiwa kutunufaisha sisi wazawa na si watu wengine hivyo ni muhimu kwenda mbele za Mungu nakumwambia Mungu kuhusu hili Taifa la Tanzania.

Askofu mkuu wa Kanisa la Tanzania Asemblies of God TAG Dk Barnabas Mtokambali

Hayo ameyasema katika sherehe za kilele ya Maadhimisho ya miaka 75 ya kanisa la Tanzania Asemblies of God ngazi ya Majimbo katika jimbo la Arusha Mashariki zilizofanyika hii jumapili ya tarehe 29 mwezi wa sita katika wa Uwanja Wa shekh Amri Abeid Karume Jijini Arusha

Aidha ameongeza kuwa kanisa hilo la TAG Lilianzishwa hapa Tanzania mwaka 1939 Igale mkoani Mbeya hivyo kilele cha Maadhimisho hayo nchini yatafanyika huko Igale mkoani Mbeya tarehe 13 mwezi wa saba ambapo mgeni Rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dk,Jakaya Kikwete Pia Askofu George Wood ambaye ni Rais Wa Makanisa ya Assemblies Of God duniani atakuwepo katika maadhimisho hayo.

Comments