EWE MRITHI UNATAKIWA UKUE.



 
BWANA YESU asifiwe ndugu popote ulipo.
Karibu tujifunze ujumbe huu wa WARITHI ambao wanatakiwa KUKUA.

Mrithi ni kinyume cha mtumwa.
Mtumwa ni mtu asiyekuwa na uhuru.
Mtumwa huamuriwa kufanya mambo hata ambayo hayataki.

Katika maisha ya mwanadamu kuna utumwa mwingi sana. Utumwa mwingine unafahamika na utumwa mwingine haufahamiki.
-Pombe inaweza kuwa utumwa kwa mtu.
-Sigara inaweza kuwa utumwa kwa mtu.
Wagalatia 4:1-7 ( Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, ingawa ni bwana wa yote; bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba.  Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia.  Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, MUNGU alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,  kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.  Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, MUNGU alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba. Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa MUNGU. )
Watoto wadogo hawakabidhiwi urithi wao hadi watakapokuwa wakubwa.
Yawezekana hata wewe leo bado ni mtoto mdogo  kiroho hivyo hufai kukabidhiwa urithi.
BWANA anataka kukuinua kihuduma lakini hafanyi hivyo kwa sababu wewe bado mtoto mdogo kiroho.
Kama kweli wewe ni mrithi please please unatakiwa  ukue.

Ndugu usikubali kuwa mtoto kiroho maana ukibaki au ukiwa mtoto kiroho kuna haki utakosa. Mfano Mama au Baba  una gari zuri sana na una mtoto mdogo na mtoto huyo anakuomba funguo  za gari ili aendeshe, hutampa maana bado ni mdogo. Lakini mtoto akikua baba yake atamwambia ‘’Mwanangu sasa unaweza kuendesha gari, nenda VETA mwezi mmoja harafu njoo uchukue funguo za gari uendeshe’’
Ndugu yangu umejifunza nini juu ya mtoto na mtu mzima. Huu ni mfano tu wa mtoto wa kimwili lakini hata kiroho wapo watoto pia na ambao haki zao nyingi hawawezi kuzipata kwa sababu ya utoto wao wa kiroho.

BWANA amekukusudia mema wewe mrithi wa ufalme wake.  Wewe sio mtumwa maana watumwa ni wale ambao hawajampokea BWANA YESU. Hawa ndio watumwa, tena ni watumwa wa shetani maana shetani ndio anawatumikisha, wengi wao ni walevi, wazinzi, waongo,waseng’enyaji, wezi  na wasingiziaji maana ni watumwa wa shetani. Hata wewe unaesoma ujumbe huu kama una tabia hizo hapo juu, basi na wewe ni mtumwa wa shetani, hujaanza kuhusika na kuwa mrithi hata kidogo. Lakini kama wewe ni mrithi basi unatakiwa ukue na sio kubaki mtoto mdogo kiroho maana ukibaki mdogo kiroho haki zako nyingi utakosa.
Kama umempokea BWANA YESU, wewe ni mrithi wala sio mtumwa.

-        Unapokuwa mtoto kiroho yanakupita mengi.
-        Paulo na Sila wangekuwa watoto kiroho wangefia gerezani. Lakini kwa sababu ni wazima kiroho na wanajua haki zao walishinda na kutoka gerezani huku watoto wadogo kiroho yaani wafungwa wenzao wao walikuwa wanashangaa tu kipindi ambapo Paulo n Sila wanatoka gerezani na wao kubaki gerezani. Matendo 16:25-34 (Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba MUNGU na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.
 Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia. Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa.Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila; kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini BWANA YESU, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. Wakamwambia neno la BWANA, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake. Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo. Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia chakula, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini MUNGU. ) .

-Kina Shedraka, Meshaki na Abednego hawakua watoto kiroho waliijua haki yao ndio maana walipona na kuwaacha watumwa wa mfalme wakifa Danieli 3 :16-22,28.(Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, MUNGU wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha. Ndipo Nebukadreza akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuru mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto. Kisha akawaamuru baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, na Meshaki, na Abednego, na kuwatupa katika ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto. Basi watu hao wakafungwa, hali wamevaa suruali zao, na kanzu zao, na joho zao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto. Basi kwa sababu amri ya mfalme ilikuwa ni kali, na ile tanuru ilikuwa ina moto sana, mwako wa ule moto ukawaua wale watu waliowashika Shadraka, na Meshaki, na Abednego. ........ Nebukadreza akanena, akasema, Na ahimidiwe MUNGU wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego; aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine, wala kumwabudu, ila MUNGU wao wenyewe. )

Ndugu yangu kama wewe ni mtumwa nakuomba kuanzia leo kataa utumwa ili uwe Mrithi yaani umpokee BWANA YESU. Na kama wewe ni mrithi, umechagua fungu lililo jema ila nakuomba jitahidi sana kukua kiroho ili usikose haki zako.

MUNGU anataka akutumie katika kazi yake lakini akikuangalia anakuona bado mtoto mdogo sana kiroho hivyo BWANA anasubiri ukue kiroho, je kama huendi kanisani, 
kama hujifunzi neno la MUNGU
 kama huombi kila siku kama 
huzijui haki zako MUNGU atakutumiaje?.   

Mtoto anaweza hata akaona nyoka kwenye TV akakimbia lakini akikua hawezi kukimbia hivyo hivyo hata wewe kama bado ni mtoto kiroho hutafaa kwa kazi kubwa ya kumtumikia MUNGU.

 Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292

                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

 MUNGU Akubariki.

Comments