FAHAMU KUHUSU BINADAMU WA AINA TATU

BWANA YESU asifiwe.

Karibu tujifunze kuhusu aina 3 za wanadamu.

 Ukweli ni kwamba binadamu wamegawanyika katika sehemu kuu tatu:- 

(1)BINADAMU WA TABIA YA ASILI 

(2)BINADAMU WA MWILINI 

(3)BINADAMU WA ROHONI. 

Na Mtumishi Alex
(A)Mwanadamu wa tabia ya asili ana sifa zifuatazo:- 

-Ni mtu ambaye hamjui Mungu yaani hajaokoka, 
-Hana Roho Mtakatifu, 
-huongozwa na shetani,
 -hufuata mambo ya kidunia. 

(B)Mwanadamu wa mwilini ana sifa zifuatazo:- 

-Ni mtu ambaye husema kwamba ameokoka lakini kwa upande mwingine hajaokoka bali ni wa mwilini, 
-Ni mtu anayejivika wokovu kwa nje huku ndani akiwa amejaa uongo na udanganyifu, 
-Ni mtu ambaye hana msimamo wa kiroho. 

 (C)Mwanadamu wa rohoni ana sifa zifuatazo:- 

-Ni mtu ambaye ameokoka na kuzaliwa mara ya pili, 
-Ni mtu anayemjua Mungu,
- Anaongozwa na Roho Mtakatifu, 
-anaweza kuishinda dhambi, 
-Ana nguvu ya Mungu, 
-Ambaye amejiandaa kwenda mbinguni, 
-Ni mtu wa rohoni. 

KWA MSAADA ZAIDI TUSOME  "1KOR 2:10-16( Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo. )

Pia tusome 1 Kor 3:1-4( Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi,  kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?  Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu? )

MUNGU awabariki sana.
By Mtumishi Alex.

Comments