FROLA MBASHA ANAKUOMBA USHIRIKI KATIKA MAOMBI YAKE




Kama unaweza kushiriki maombi haya pamoja nami, Mungu akukumbuke, na kama upo kwa ajili ya kuhukumu, pia Mungu akukumbuke. Math7:1 Msihukumu msije mkahukumiwa ninyi, kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayo hukumuwa; na kipimo kile mpimiacho ndicho mtakacho pimiwa.
Math5:44 Lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.
‘ Mungu wewe ni Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu. wewe ni Mkuu sana, wewe ni mwanzo tena mwisho zaidi yako hakuna na hatakuwepo. umesema ktk 1wathesalonike5:18 shukuruni kwa kila jambo maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu ktk kristo Yesu. ahsante Mungu maana wewe uliijua jana yangu, leo na kesho itakuwaje.Mungu wa amani unitakase kabisa nafsi yangu, mwili wangu na roho yangu unihifadhi, wewe BWANA ni mwaminifu.

Ktk Isaya43;19 umesema,Tazama nitatenda neno jipya: sasa litachipuka je hamtalijua sasa? nitafanya njia hata jangwani na miito ya maji nyikani. BWANA mapenzi yako yatimizwe, tenda lililo kusudi lako juu yangu. ktk Math14:14 umesema, mkiniomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya. ukasema ktk Marko10:27 Yesu akawakazia macho akasema, kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo: maana yote yanawezekana kwa Mungu.

Maombolezo3:31-32 Kwa kuwa BWANA hatamtupa mtu hata milele, maana ajapo mhuzunisha atamrehemu kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.
Mungu inua moyo wangu sasa, wewe ndiyo msaada pekee wa kweli. Ninaamini utatenda makuu kama ilivyoandikwa ktk Zaburi 108;13 Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, maana yeye atawakanyaga watesi wetu. Bwana wewe ni mtu wa vita, Bwana ndilo jina lako,pigana sasa ninakuachia wewe.
ninashuka mbele zako ninaungana na wenye uhai wanne ktk Ufunuo4;6-11 kukuabudu wewe nikisema, 11 Umestahili wewe BWANA wetu na MUNGU wetu,kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako navyo vikaumbwa.
Zab23;4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami.
AMEN

Comments