HABARI PICHA: SAFARI YETU YA KIHUDUMA CHALINZE.


Siku chache zimepita ambapo MUNGU alinipa neema ya kwenda Chalinze kama viongozi wa vijana wa kanisa letu la P A G. Katika safari hiyo tulikuwa ni Akofu Thomas Dige ambaye ni Askofu wa jimbo la Dar es salaam P A G, Askofu Joseph Masanja ambaye ni mkurugenzi mkuu wa idara ya vijana taifa na ambaye pia ni Askofu msaidizi wa P A G jimbo la Mwanza. Pia alikuwe Mchungaji Lucas Mpenzile ambaye ndiye mkurugenzi wetu wa vijana jimbo la Dar es salaam. pia alikuwepo Joseph Mao ambaye ni mkurugenzi msaidizi pamoja na mimi ambaye ni katibu wa vijana jimbo.
Haya ni baadhi ya matukio katika picha katika ziara hiyo ya chalinze.

Ubungo tayari kwa safari. Kutoka kushoto ni Joseph Mao, Askofu Masanja na Mchungaji Mpenzile.

Tumefika Chalinze.

Wakati wa kumsifu MUNGU

Mimi ndio nilikuwa kiongozi wa semina hiyo ambayo iliwakutanisha makanisa mawili, kanisa la Chalinze mjini na kanisa la Buyuni.

Kumtumikia YESU ni raha maana utakutana na watakatifu wa aina mbali mbali. Hapa ni mimi nikiongea jambo wakati wa ibada.

Mkurugenzi wa jimbo wa vijana akisisitiza jambo.

Askofu Masanja akisalimia na kutoa mwongozo wa vijana katika kanisa.

WALINIBARIKI SANA WATEULE HAWA AMBAO NI WAMASAI, NILIBARIKIWA NAO  SANA MAANA WANA MPENDA YESU SANA
KWAYA WAKIINGIA KUIMBA.



HII KWAYA INABARIKI SANA.

Askofu Dige tayari kwa kufundisha somo liitwalo UCHUMBA NA NDOA

Comments