HAKUNA KURISTI(NO RECEITORS) KATIKA HUKUMU YA MUNGU.

Ni wakati wa shule ya wokovu muda huu ili tushinde mitihani yaani dhambi na mambo ya dunia

Ebr 9:27

INASIKITISHA MNOO! TENA MNOO! KWA WATU WANAODAI WAMEOKOKA LAKINI WANASHINDANA NA MAAGIZO YA MUNGU.

  Mtu ameokoka lakini anaukataa Ubatizo wa Maji Mengi(tele)! Ni ajabu mnoo!
Mt 3:13-15

Utashangaa mtu anatetea mavazi ya kikahaba, eti anadai Mungu haangalii nje bali ndani (Roho) Wengine wanajiita Wachungaji, Maaskofu, Manabii, Mitume na Wengine wainjilisti nk
Mithali 7:10

Utashangaa mtu anafikia hatua ya kujibadili rangi yake ya asili,(KUJICHUBUA) na hapa utawakuta hata hao wanaojiita Watumishi wa Mungu! nao wamo katika mkumbo huo huo! Kama hao waimbaji wa Nyimbo za Injili ndo usiseme! Sasa sijui wanawafundisha nini waaminio na wasio amini! Rumi 9:20, Isaya 29:16

Nilishangazwa na Mchungaji mmoja wa KIUME! Yeye anapaka colour less(Ile rangi ya kung'arisha kucha) kwenye kucha zake!
Sasa sijui huo ni urembo??? au anafanya hivyo ili iweje!!! Bila shaka hili andiko limekaa kushoto naye
2Kor 3:2-3

Mpendwa wangu katika Kristo, USIDANGANYIKE! Kuokoka siyo fashion bali ni kujikana nafsi! (KUGHARIMIKA) Unauchukua mzigo wako mwenyewe Gal 6:5 na siyo wewe na Mchungaji wako laa hasha,ni wewe peke yako!

Sipati Picha ikiwa utakuwa umezishika amri zote Mt 19:16-21
Lakini ukajikwaa katika jambo dogo kama ubatizo! Pale utakapoambiwa umefanya yote lakini hukutii agizo lingu la kuitimiliza haki YOTE
Mt 3:15

Mpendwa wangu katika Kristo, kwa Mungu hakuna kurudia (Kwenda kusafisha cheti, yaani kutubu dhambi ulizojichanganya) Ukikosa, Umekosa juu ya yote Yak 2:10

Hivyo ni heri kusafisha cheti chako hivi sasa kabla ya HUKIMU! Ukiona bado unatamani masuruali, kujichibua, mirasta, mikobe ya bandia, mikucha ya bandia, lipstick, nk... ni heri umwombe Roho wa neema akusaidie vinginevyo utapotea jumla!

Mpendwa wangu ni bora kuachana na vyote hivyo kwani hakuna palipoandikwa ukiviacha ni dhambi bali ukivitumia halafu ukakuta Mungu yu mbali navyo itakugharimu sana!

Kimsingi hatuwezi kuacha hayo yote kwa nguvu zetu bali ni kwa Neema mtu yoyote asikudanganye! Binafsi nimewezeshwa na Mungu muweza wa Yote, na nimeweza na bado naendelea kuomba aninoe zaidi na zaidi. Efe 2:8-9

Wewe jiulize na kujihoji mwenyewe pale Bustani ya Eden,Adam alifanya dhambi gani kubwaa?? Au dhambi ngapii?? Zaidi ya dhambi moja tuu ya KUTOKUTII??
Aliambiwa USILE... YEYE AKALA
Mwa 2:16-17

Musa halikadhalika, Pamoja na kuwa rafiki wa Mungu wa karibu sana, lakini kwa kosa moja tu hakuweza kuwaingiza wana wa Izrael Kanani
  Aliambiwa UAMBIE MWAMBA utoe maji! Badala ya kuuambia mwamba yeye akapigaMWAMBA!
Hes 20:7-12

Mpendwa wangu katika Kristo ikiwa wewe umeamua kumfuata KRISTO basi tii kila agizo aliloliagiza, waswahili husema ukiambua kula nguruwe ule na Pua yake!
  Tusizidiwe akili na wasio tahiriwa! Bali haki yetu izidi hao mafarisayo Mt 5:20

Biblia inasema mwenye kujitakasa na azidi kujitakasa na mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu....Ufu 22:11-12

Itakuwa haina maana kujichanganya changanya! Kwani huko ni kujinyima uhondo,na uhuru kamili, kumbuka biblia inasema vuguvugu watatapikwa Ufu 3:16

Hivyo nikushauri mpendwa wangu acha tabia ya kuweka mguu mmoja kwa Yesu na mwingine kwa Shetani! Hutoweza kuvipata vyote kwa wakati mmoja, utaratibu ni KUCHAGUA MOJA TU! Sasa angalia usijicheleweshe, kama umechagua ya dunia tia bidii maana baada ya maisha haya huna chako tena, nawe Mteule wa Bwana jilinde na yote ya dunia hii, kwani bado kitambo tuu utastarehe milele!

Ila ni maombi yangu kwa BWANA usimame upande wa MUNGU kwa kutenda mema na utii mbele za MUNGU WETU maana kuna faida! Kumb 30:15-16

Ahsante kwa kusoma ujumbe huu!
Baraka za Bwana ziwe nanyi nyote! 

Shaloom Shaloom!
By Lucy Marandu.

Comments