JIBU LA NDOA YAKO.

Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania


Bwana Yesu asifiwe!
Napenda kukukaribisha katika somo hili juu ya ndoa.

¤Mwasisi wa ndoa ni Mungu mwenyewe(Mwanzo2:18-24)
¤Ndoa-Ni muunganiko wa maisha matakatifu kati ya mtu mke na mtu mume kwa mamlaka ya Mungu kupitia kanisa.Maisha haya huwashirikisha wazazi wao wa kimwili na wa kiroho pia.

¤Nini maana ya MUUNGANIKO WA WAISHA?
¤Maana yake ni usawazisho wa kukubaliana kuweka maisha binafsi(individual life)pamoja na kuyagawana(to share)kwa pamoja.Hii inamaana kuwa watu hawa wawili wanaweka mapatano/mkataba au agano la kuunganisha maisha yao i.e. biashara zao,akili,umasikini,urembo,mali,akaunti zao,magonjwa,dhiki,madeni nk ktk kudumisha maisha ya milele.
¤Lazma wanandoa watambue wao ni mtu mmoja japo ni miili tofauti.

¤Misingi ya ndoa ni ipi?
¤Ndoa yoyote ile hutegemea mambo makuu manne ambayo ni *UPENDO,*FURAHA,*UAMINIFU&*UVUMILIVU.

Je,misingi hiyo hupaswa iweje?mbona bado ndoa nyingi zinaangamia wakati upendo,furaha nk vipo?


VYANZO 6 VYA MIGOGORO KTK NDOA.

Ndugu wapendwa,hakuna bingwa wa ndoa duniani hata kama amemudu kuishi na wake wengi kiasi gani.
Suluhisho kamili la migogoro yote ni kumkabidhi Yesu ndoa yako.

*Mawasiliano>mtandao wa kupashana habari ni suala la muhim sana.njia hii huwaleta watu karibu muda wote.
*Mapatano>hii inamaanisha kulitunza agano lenu kwa nguvu zenu wote na kwa gharama yo yote.
*Majukumu>katika mgawanyo wa kazi,kila mwanandoa anapaswa kujiona anapaswa kuwajibika kwaajili ya familia yao na wala siyo kutegeana.
*Imani>misimamo binafsi ya kiimani,dini au mila na desturi ni muhimu sana zikawiana baina ya wanandoa hawa wawili.epuka misimamo ya upande wowote baina yenu.
*Uchumi>gawanyo la mapato linapaswa kuwa ktk matumizi mlioafikiana kwa manufaa yenu wote.haifai kutumia ubabe au kujitangazia umiliki.
*Hisia mbaya>hali ya wasiwasi na mashaka si suala jema ktk maisha.ni vema mkawa wa wazi na wakweli daima.
Ndg wapendwa,msiruhusu ndugu,jamaa wala marafki kuwaamulia juu ya ndoa yenu na jihadhalin nao


 Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.
Kwa Mobile +255(0)7 (57/84) 464 141/ 12 909 021.
Au Email sos.sesi@yahoo.com / newelshaddai@gmail.com

Tunakushauri, utembelee kanisa la kiroho lililo jirani yako, kwaajili ya mafundisho zaidi na Ushirika. (Kumbukumbu la Torati 28:6).


Comments