JINA LA YESU NDILO JINA PEKEE TULILOPEWA.

Jina La YESU KRISTO Ndilo Tulilopewa.

Hatulijui Jina Jingine Maana Tuliyajaribu Majina Mengine Yote Kabla Hatujaokoka Tukagundua Hayana Uwezo Wa Kuokoa, Tena Majina Ya Watu Hao Wote Kwa Sasa Ni Marehemu Hivyo Tukashindwa Kulitumainia Jina La Marehemu. Ila YESU Tu Maana Yuko Hai Milele.

 Kuna Muda Fulani Tulitumainia Majina Ya Watu Walio Hai Mfano Waganga Wa Kienyeji Tuligundua Wote Ni Matapeli Na Ni Mawakala Wa shetani Na Ambaye Ndiye Aliyetuletea Matatizo Hayo. Kumbe Hakuna Jina Jingine Ambalo Tunaweza Kupata Msaada Ila Ni Jina La YESU KRISTO Pekee. 

MUNGU BABA Mwenyewe Anasema Neno Hili Wakati YESU Akianza Huduma Yake Duniani " Huyu Ni Mwanangu, Mpendwa Wangu, Ninayependezwa Nae- Mathayo 3:17 

Na Tena BWANA MUNGU Akawaambia Mitume Mbele Ya YESU Neno Hili " Huyu Ni Mwanangu Mpendwa, Ninayependezwa Nae Msikilizeni Yeye- Mathayo 17:5 

Na Wewe Ndugu pamoja na mimi naomba tusome  Wafilipi 2:5-11( Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya KRISTO YESU; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya MUNGU, naye hakuona kule kuwa sawa na MUNGU kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;  bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena MUNGU alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la YESU kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa MUNGU Baba. ). 

Ndio Maana Tunadiriki Kusema Kwamba " HUKO(kwa shetani) TULITOKA NA SASA TUKO HAPA(KWA YESU) , TUNATANGAZA WEMA WA BWANA ALIYETUOKOA. Asante YESU
  Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisha kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292

                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

 MUNGU Akubariki.

Comments