JOSEPHAT MWINGIRA: JINSI NILIVYOTOKEWA NA BWANA YESU.


Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat  Mwingira

BWANA YESU asifiwe.
Kuanzia leo nitakuwa nakuletea ushuhuda wa mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Mwingira Mbeba maono wa huduma ya Efatha.
Ushuhuda huu pia upo katika kitabu ambacho Mtumishi wa MUNGU Josephat Mwingira amekiandika kinaitwa WITO WANGU.
  
karibu.  

Nakumbuka siku moja, nikiwa Mererani huko Arusha, BWANA YESU alinitokea chumbani. kwakuwa nilikuwa mzinzi na mlevi niliyebobea, ndiyo kwanza nilikuwa nimetokea kwenye starehe zangu, tayari nikiwa na dada mmoja kahaba. YEYE akaniambia anataka niache hayo maovu kisha nimtumikie YEYE. Kama nilivyoeleza hapo juu, mimi nilikuwa katika mazingira ambayo hayakuwa mazuri sana kwa sababu nilikuwa katika hali ya ulevi na mshiriki wa mambo mengi ya dunia.
Yule dada alipoona hali hiyo akakimbia, nikabaki (Josephat) peke yangu. BWANA YESU akasema, “Mimi ninakutaka wewe uache maovu yote na unitumikie.”. baadaye wakati alipotaka kuondoka, ikanibidi nimshike miguu na kumng’ang’ania, nikamwambia, “usiniache!” akashuka chini na kunishika bega la mkono wa kulia akasema “nitakuwa na wewe “ Halafu akatoweka. 

Baada ya hapo yakawa yananitokea maono Fulani Fulani ya kutumwa. Mara BWANA YESU alinituma nikawaombee watu Fulani Fulani waokoke au wapone kutokana na magonjwa yao wakati mimi nilikuwa bado sijui kuokoka kilikuwa kitu gani. Lakini nikawa Napata neema ya kwenda kuwaombea na wagonjwa wakawa wanapona. Wakati mwingine BWANA YESU akawa ananitokea katika ndoto au anatuma malaika ambao walikuwa wananielekeza watu wa kwenda kuwaombea uponyaji kutokana na matatizo yao. 

Kufikia hapo nikawa, hata nikienda kunywa pombe, nilikuwa naitapika yote. Hamu ya pombe ikaisha na nikaichukia moja kwa moja. Na baada ya hapo, nikawa nasukumwa kuomba kila wakati ndani ya nafsi yangu japo nilikuwa sijui hata kufungua Biblia, ukiachilia mbali kwamba nilikuwa sina Biblia. Kwa asili, mimi nilikuwa Mkatoliki – nilizaliwa huko, nikabatizwa huko na nikakulia kwenye mazingira ya Kikatoliki ambako waumini wake hawana kawaida ya kusoma Biblia. lakini nilipokwenda Arusha, nikajikuta naabudu na walutheri kwa sababu marafiki zangu wote niliokuwa nasali nao wakati huo, walikuwa walutherani.  

Wakati huo nilikuwa nakijua kitabu kimoja tu kiitwacho “NYIMBO ZA KIKRISTO” na nilikuwa naujua zaidi wimbo mmoja tu katika kitabu hicho unaitwa “NJOONI KWA MPONYA” ….
Nilikuwa naupenda sana ule wimbo lakini sikujua ni kwa nini nilikuwa naupenda. Lakini baada ya maono haya, niliendelea hatua kwa hatua na namshukuru sana MUNGU kwamba leo ninaelewa vizuri kwa nini nilikuwa naimba
NJOONI KWA MPONYA’.
Baada ya hapo nikawa nawiwa kwenda porini mara kwa mara. Siku moja, nikiwa naomba, nikasikia sauti inaniambia, “Nenda, kajitenge, ukakae porini kwa muda wa siku saba!” Nikaenda porini kuomba kama nilivyoelekezwa. Nilikaa huko siku ya kwanza, siku ya pili, siku ya tatu, na ilipofika alfajiri kuaamkia siku ya nne, nikasikia sauti zinaimba;
“Ee, MUNGU wetu; tunakuabudu!” itikio, “Tunakuabudu.”
“Ee, MUNGU wetu; ndiwe BABA yetu!” itikio, “ndiwe BABA yetu’.
“Ee, MUNGU wetu; ndiwe MUUMBA wetu!”
Itikio, “Ndiwe MUUMBA ….wetu.”
Kiitikio,   “Ndiwe MUNGU wetu”.
“Ndiwe MUNGU wetu”.
“Ndiwe MUNGU wetu”.
“Ndiwe MUNGU wetu”.

ITAENDELEA........
Usikose sehemu inayofuata ambapo mtumishi wa MUNGU anachukuliwa na malaika hadi mbinguni. Je nini kitaendelea huko.
Usikose hapa hapa Maisha ya ushindi blog. 



Comments