Kwa mara nyingine tena imejidhihirisha kwamba kundi la Joyous Celebration linamashabiki wengi zaidi Afrika magharibi baada ya kuwa Ghana mwaka jana, kwa mara nyingine kundi hilo limeondoka usiku wa kuamkia hii leo kuelekea nchini Cameroon ambako wanamwaliko wa kihuduma uliopewa jina la Joyous Celebration Festival ikiwa ni mwendelezo wa mialiko kutoka Afrika magharibi.
Katika msafara huo kundi hilo limeongozana na waimbaji wake wa zamani
akiwemo mwanadada anayependwa sana na mashabiki wa Joyous Mahalia
Buchanan a.k.a Hally, Unathi Mzekeli pamoja na
![]() |
Pastor Patrick Duncan. |
mchungaji Patrick Duncan ambaye toleo la 15 lilikuwa ndio toleo lake la
mwisho na kundi hilo, ambapo inaelezwa kwamba kuambatana na kundi hilo,
kunatokana na watu waliolialika kundi hilo kutaka waongozane na mwimbaji
huyo ambaye uimbaji wake katika kundi hilo ulikuwa umelalia katika
mapigo ya kimarekani na kuabudu ambapo tangu aondoke bado hajapatikana
mwimbaji anayeimba aina ya utunzi wake.
Joyous ambayo ina mashabiki wengi zaidi nchini Afrika ya kusini na nchi
jirani, tayari imeshatangaza ratiba ya maonyesho yake kwa mwaka huu
katika kuitangaza DVD yao ya 18 iitwayo One purpose ambayo wiki ya
kwanza toka ianze kuuzwa ilipokea upinzani mkubwa kutoka kwa mashabiki
na wapenzi wa muziki wakilalamikia kwamba haikuwa nzuri kama
walivyotarajia kutokana na kundi hilo kuimba nyimbo nyingi za makanisani
na sio nyimbo mpya walizotunga wenyewe, huku pia zikitengenezewa mziki
mgumu jambo ambalo lilipelekea aliyekuwa malkia wa kundi hilo mwanadada
Ntokozo Mbambo wa Mbatha kuwapiga marufuku mashabiki wanaoponda kazi
mpya ya kundi hilo kuandika ujumbe kwenye wall yake ya Facebook kwakuwa
wanamuumiza na Joyous ni familia yake. Aidha uamuzi wa mwanadada huyo
ulikuja kutokana na wengi kuanza kumtaja Nqubeko kwamba angefaa
kuendelea na kazi ndani ya Joyous na sio muongozaji mpya Siyanqoba
Mthethwa.
![]() |
Mahalia Buchanan akiwa mazoezini na Joyous hapo jana tayari kwa safari na Joyous. |
![]() |
Unathi akiwa na Sylvester wakati wa mazoezi ya kundi hilo hapo jana. |
![]() |
Sylvester katikati akiwa na waimbaji wenzake ndani ya ndege wakielekea Cameroon. |
Wakati huohuo wakati Joyous wakiwa nchini Cameroon, Ntokozo na mumewe Nqubeko watakuwa nchini Ghana wiki ijayo kwa mwaliko wa kihuduma ikiwa ni mara yao ya pili mara baada ya kuwa nchini humo mwaka jana
Chanzo: Gospel kitaa
Comments