KAMWE SI MAZINGIRA YATAIBADILI BIBLIA BALI BIBLIA NDIYO ITABADILI MAZINGIRA



Neno linatwambia:
"HAKUNA JIPYA CHINI YA JUA"
Mhubiri 1:9

Huwa nashangazwa na watu ambao wanatetea dhambi kwa madai kwamba eti yapo mazingira yanayomlazimu mtu kuishi kulingana na Mazingira yenyewe! Mfano Joto baridi nk

Wamesahau neno hili: JE NI NINI/NANI ATAKAYE TUTENGA NA UPENDO WA KRISTO?? Je ni dhiki, au shida, au adha, au uchi, au hatari au upanga??
Rumi 8:35.


Nikiwa katika kumhubiri Kristo, Nikakutana na watu kadhaa, nikawashirikisha neno la Kristo! Kisha nikagusia kwa habari ya Mavazi! Kulingana na walivyovaa!

Wakadai mavazi siyo jambo la kuhubiri kwani ukienda sehemu kama Marekani na maeneo mengi ya Ulaya culture yao huvaa suruali kwa wanaume & wanawake kwa sababu ya baridi nk!

Wakanitajia sehemu nyingine, nimeisahau wanasema katika nchi hiyo culture yao, watu wote huvaa magauni, wanaume kwa wanawake!(Siyo kanzu) bali magauni hasaa!!

Kwa kuwa walikuwa wanaume na wanawake, nikawauliza wale wanaume, Kwa hiyo kwa kuwa wale wanavaa magauni ninyi nanyi mwataka kuvaa vivyo hivyo??
Wakacheka wote, mmoja akasema siyo sisi tuvae bali huo ni mfano tuu,ili uone siyo issue!

Sasa nikawauliza; Kwani ninyi ni wa Imani ganii?
Wakajibu ni Wakristo

Jee mwongozo wenu wa kuwadhibitisha kuwa ninyi ni wa Kristo ni upii??
Wakajibu ni Biblia

Sasa ikiwa ni Biblia? Je tuziangalie nchi za magharibi zinavyoenenda au tuenende kama biblia ututakavyoo tuenende???
Kimyaa!!

Ni nani aliye juu ya biblia basi?? Ikiwa watu wanatii katiba za nchi zao na hakuna hata mmoja anayeweza kuwa juu ya sheria ya nchi, Je si zaidi sana sheria ya Mungu??
Kimyaa!!

Wapendwa wng katika Kristo tusidanganyike, Wazungu sii lolote sii chochote juu ya Mungu! Kumbuka ushoga umeanza kidogo kidogo na sasa unaenea kwa kasi ya ajabu duniani kote, Na umeanzia huko kwao!

Biblia inasema; Au hamjui ya kuwa WAFIRAJI, WALAWITI, WAZINZI nk hawatauridhi ufalme wa Mungu?1kor 6:9

Je tumsikilize Mzungu kuliko Mungu??

Na mavazi vivyo hivyo walianza visuruali,mara vikaptula, mara vichupi nk, kwa madai wanaenenda kulingana na majira
(baridi & joto)

Lakini biblia inasema, Msienende kama ulimwengu uenendavyo Rumi 12:2

NA HUU NI UONGO WA SHETANI TUU!
Ikiwa wapo watu ambao hawajaokoka, na wanavaa gubi gubi na kuacha macho tuu, ina maana wao hawaoni joto? Sisemi watu wavae gubi gubi lakini ni muhimu kujua imetupasa kuwa Kielelezo kwa wasio amini! Sasa ikiwa wasioamini ndo wamekuwa kielelezo kwa waaminio hii inatisha kama nini!

Waaminio tupo bize na fation, tumeyaacha maziwa nje kwa madai tupo ndani ya top! Viuno nje, michoro halisi ya maumbile yetu Mmmmmmh!
Hakika inasikitisa!

Mungu tusaidie....

Shaloom Shaloom!

By Lucy Marandu.

Comments