![]() | ||||||||||||
Habari ndugu
mchungaji,kuna document ambayo nilikutumia kwenye email yako, uliiona? Ile document imeniongezea sana imani kwani mengi niliyopitia nilipata
kujulishwa kupitia ujumbe wake wakati nasoma form 5 nikastaajabu sana yale yaliyomo
hata leo nakiri kuwa MUNGU alinionesha hatari zote awali kabla hazijatokea .Najua
ahadi yake kwetu haiwezi kuyumbishwa na dhoruba yoyote tunayoweza kuieleza
kibinadamu. Naamini
salama ambayo MUNGU hutupatia katika hatari ambazo hatuwezesha kushinda.
Kwa hali ya
kibinadamu Dunia imejaa dhoruba zenye kukatisha tamaa nazo huletwa na
ndugu,rafiki,jirani hata wazazi lakini ushindi upo katika MUNGU wetu, tena yeye ana nia njema,tudumu kumtanguliza yeye katika
mipango yetu.
Hakika MUNGU
anajibu magumu tunayopitia. Nakumbuka
mwaka 2008 wakati nimemaliza form 6 nasubiri matokeo MUNGU alinionesha jambo kuu,niliamka mapema kama saa
kumi na moja kasoro kujiandaa kwenda kuchukua cheti changu cha form 4 ndipo
wakati nikipasha maji moto ili nioge maji yalivyochemka nikawa natoka jikoni kwenda
kuchukua ndoo ya kuweka maji,lakini wakati natoka nikazima taa kabla ya kutoa
mguu pale mlangoni wazo likanijia kuwa ‘’rudi uwashe taa usiache jiko likiwa
giza’’ ndani ya sekunde ile nikatii, wakati nageuka kupeleka mkono kwenye swich
nikaona mwale wa mwanga kama kijinga cha moto nikasema huo ni mwangwi tu kwani
nilikuwa kwenye mwanga,hivyo sikutishika kitu ila wakati nageuka kutoka jikoni
pale mlangoni nlipotaka kukanyaga ndipo nikamwona nyoka anagalauka huku
anametameta na hii hali ndiyo iliyonifanya nimwone kwani pale mlangoni hapakuwa
na taa ila ile nuru ndio iliyosababisha nikamwona yule nyoka,sikutishika bali nikajiuliza swali
moja kuwa nini kinatokea nikahoji nafsi yangu kipi kiliniongoza nisikanyage nje
nikatii ile sauti iliyonijia,kwanini namwona huyu nyoka katika hali hii lakini
awali sikumwona na wakati nataka kukanyaga pale wazo linanijia ndani ya sekunde
na kulitii bila kuhoji ndipo nasema hakika MUNGU amekuwa nami katika hila zote
za ibilisi dhidi yangu na familia pia Ndipo siku moja wakati nilipowiwa kumsimulia
dada mmoja tuliyekutana chuoni akaongozwa kuongea haya,"Dickson MUNGU
anakupenda sana ndio maana humtuma malaika wake kukuokoa katika hatari zote,akasema hata kutii ile sauti moyoni mwako akasema hata ile nuru iliyopatikana kwa
kuwasha taa ilibadilishwa kuwa nuru ya rohoni ndio maana uliweza kumwona yule
nyoka katika hali tofauti kwani macho ya rohoni yamepewa nuru kwa kutii sauti
ile. Nilitumia maji yaliyobarikiwa kwa maombi yule nyoka akatoweka bila kuacha masalia
yoyote BWANA amenionesha makuu ndugu na ahadi zake ni bayana kwetu kwani
hutuongoza katika hatari zote huwa kama kuna hatari fulan inakuja nachelewa
kupata usingizi na mara zote nakuwa busy kupitia vifungu anuai katika Biblia Nakumbuka
nilikuwa ninasoma bible ndipo ukanipitia usingizi muda wa sa 8 usiku
ilipokaribia sa 9 nikajiwa na maono ambapo nikaamshwa na kuoneshwa jambo naoneshwa
kibwengo mithili ya mzee wangu anaingia chumbani nilipolala lakini mkono mmoja
upo kwa nyuma,nikawa natizama tu kuwa kitafanya nini? kikawa kinasogelea zaidi kitanda
ambacho nililala huku mkono ukiwa nyuma,nikawa siogopi bali kuangalia kitu gani
kingeendeleaindipo kikaanza kuurudisha taratibu ule mkono kumbe kilikuwa
kimeficha kisu,lakini sikupata hofu kwani nilikuwa naoneshwa hatua moja hadi
ingine, kilipojaribu
kunichoma kisu kifuani nilipaza sauti kali ambapo wazazi wangu walipata hofu
kuu wakashindwa kufika pale chumbani nikawasihi wasihofu waje niwasimulie ila
vitu vilivyokimbia huko nje kwa mshindo mkuu baada ya ile sauti Ndipo walifika
wakiwa na hofu kuu nikawasimulia basi nakaendelea kulala hadi saa kumi na 1
ndipo ikanijia ndoto hii, nimetoka shamba na mbwa wetu(alikuja na kufanya makaz), kabla ya kufika
home akatokea mbwa mwingine ghafla na kumng'ata shingoni yule mbwa nliyekuwa
nae,wakati naduwaa kwa ile hali kwani mbwa yule alitokwa damu nyingi hata
kulegea wakati nasubiri mbwa afe nione kuwa ataning'ata mimi au vipi
nikashangaa kuona na yule mbwa aliyemng'ata mbwa wangu amefia pale
pale,nikaongozwa katika tafsiri hii huyu mbwa aliyekuwa nami ni ndugu wa karibu
lakn si mwema kwangu na familia yetu,na huyu aliyevamia na kumng'ata ni watu
wengne wanaonifahamu vema na familia yetu lakini ubaya wao ni shirika moja na
huyu aliyekuwa karibu kama ndugu. Ndo maana wakati nawaza kuwa atanidhuru
akafia pale na kuniacha
MUNGU
aliniokoa maana nyoka Yule alikuwa anatisha sana na hakika sijui ingekuwaje
lakini MUNGU aliniokoa. Pia mbwa Yule alikuwa anatisha lakini MUNGU aliniponya
hata kibwengo alikimbia.
MUNGU
akubariki sana.
Dickson
Haji.
Morogoro.
|
Comments