KIONGOZI ANAVYOTAKIWA AWE.



Photo: APOSTLE N PROPHET MWINGIRA
Na mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Mwingira
Kiongozi akiwa amejaa Roho Mtakatifu ni vigumu kumuelezea lakini ukimkaribia unaona ile nguvu ya Mungu na ile nguvu ya Mungu inakuwa kama harufu nzuri yenye kuvutia, mtu huyo akiwa na hiyo nguvu ni rahisi kubadiri mazingira yoyote yanayomzunguka na hata kusababisha wale wanaomzunguka kubadili mazingira yao; 1kor 2:1-5
Imani yetu katika Kristo lazima ionyeshe nguvu ya Mungu na matendo ya Roho Mtakatifu, nguvu ndiyo itakayoonyesha mabadiliko yako wewe binafsi , ndiyo itakayomfanya shetani akae mbali na wewe, Neno la Mungu linasema, takeni sana kuwa na karama za Rohoni nguvu hii itasaidia kuleta mabadiliko kwa hao utakaowaongoza.
Neno la Mungu katika mithali linasema 'Yeye azimiae wakati wa shida nguvu zake ni chache' changamoto ikikutokea ukaona unakata tamaaa basi wewe nguvu zako ni chache!
Kiongozi ni sababisho la kila kitu sasa kama huonyeshi majibu, basi hao unaowaongoza watakuonyesha jibu,jitie nguvu kwa Bwana kama mfalme Daudi alivyofanya.

Kiongozi lazima alete majibu, katika kila mtu aliyeumbwa na Mungu kupitia mazingira tulikozaliwa kuna asili fulani ya uongozi ndani ya mtu sasa ukiweza kubaini hicho ndani ya mtu utamtumia lakini kwa sababu hatujaweza kubaini basi hizo aina flani za ujuzi wa uongozi vitakaa tu.. visitumike.

Mambo 4  ya kuchochea uongozi wako

1. Ainisha mapungufu yako mambo yapi umeshinda na yapi umeshindwa kisha ukishirikiana na Roho Mtakatifu ambaye ndiye Roho wa nidhamu yaainishe hayo maeneo ukimshirikisha Roho Mtakatifu ambaye ndiye Roho anayetuongoza zingatia zaidi kwenye maeneo, tambua namnagani utakabiliana na upinzani na sio kulia wakati frani kunamadhaifu katika mwili , kama mwili umefanya vibaya kisha mwambi Roho akusaidie wekeza zaidi katika maeneo unayofanya vizuri hakikisha kwenye madhaifu ukiyarekebisha mapungufu yote uliyoyabaini, mfano eneolako unalofanya vizuri ni lile la upinzani

2. JINSI YAKUTHIBITISHA KUONGEZA NGUVU; fanya maombi ya mara kwa mara hayo maombi utakayoomba ni maombi ya kubatilisha yale mapungufu yako ukamilishe mfano kiri ushindi katika kutaka kushinda na hayo maombi yanakuwa ni ya kwako binafsi katika udhaifu wowote mshirikishe Roho Mtakatifu na hiyo ndiyo iwe tabia yako

3. CHOCHEA KIPAWA CHAKO CHA UONGOZI KUSHINDA MAPUNGUFU kama ni kushindwa sema kushindwa hakuta kaa na mimi fanya kwa nguvu na kwa bidii sana kwa sababu kushindwa ni roho huwezi kushinda bila Neno la Kinabii na la mamlaka ili kukuachie hakuna kitu kitatokea unakuta kila siku unarudishwa nyuma tu hata kama ni maradhi yatamkie.

4. UWE MWANGALIFU WAKATI SHUTUMA ZINAPOJITOKEZA; uwe makini katika kuzuia na sio kuhamaki;

Comments