KIPINDI CHA PILI CHA SAFARI YA NDOA

Na Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministries (VHM).

VIPINDI VITATU VYA SAFARI YA NDOA!
1. MUME NA MKE WAWILI TU KATIKA NDOA KABLA YA KUPATA WATOTO - MIAKA 3 YA KWANZA

2. KIPINDI CHA KUZAA WATOTO NA KUKUZA WATOTO - MIAKA 25 - 35

3. KIPINDI CHA MWISHO MUME NA MKE WAWILI TU, WAKATI WATOTO WOT...
KIPINDI CHA PILI CHA SAFARI YA NDOA
Kipindi cha Kupata watoto na Kukuza watoto – Miaka 25 hadi Miaka 35.
1. Kuanzia kipindi cha mimba na mpaka kupata mtoto/ watoto ile furaha na burudani ya tendo la ndoa huingiliwa na kupunguzwa thamani yake kutokana na majukumu sasa ya kulea watoto.

2. Kuna baadhi ya wanawake wakipata tu minba zinakuja na changamoto zake. Wengine wanapewa “bed rest” wengine wanakuwa wadhaifu kuanzia mwanzo wa mimba mpaka kujifungua.

3. Sasa kama ndio tu mmeoana na mke ndio amepata hizo “complication” zinazomzuia asishiriki unyumba na akishajifungua macho yake yote yanahamia kwa mtoto mume atateseka sana na huo hautakuwa msingi mzuri wa ndoa.

4. Katika kipindi hiki “attention” huhama au hugawanyika kutoka kwa mume kwenda kwa watoto.

5. Katika kipindi cha kwanza mke hujitahidi kutoa “attention” yote kwa asilimia 100 kwa mumewe na mume kwa mkewe.

6. Katika kipindi cha mimba na hasa mtoto anapozaliwa “attention” huamia kwa asilimia 90 kwa mtoto na alisimia 10 tu ndio hubakia kwa mumewe.

7. Hiki huwa ni kipindi kirefu san asana kwani kinachukumu muda mwingi wa wanandoa kushughulika na watoto zaidi kuliko kushughulika kwajili yao wao wawili.

8. Kipindi hiki huchukua kati ya miaka 25 hadi 35 mpaka watoto wote wanapokuwa wamehama kutoka katika himaya ya waazi wao.


MUNGU akubariki sana pia samahani kwa kuanza na sehemu ya pili, sehemu ya kwanza itakuwepo hapa kesho.

Comments