KONGAMANO LA VIJANA MBEYA NA MCHUNGAJI MITIMINGI; MAELFU WAHUDHURIA.

Mchungaji Peter Mitimingi akifundisha.


Mamia ya vijana kutoka mkoani Mbeya na vitongoji vyake walifurika katika ukumbi wa shule ya St Mary uliopo Forest jijini humo, kusikiliza mafundisho yaliyokuwa yakitolewa naa mkurugenzi wa huduma ya The Voice of Hope ministries (VHM) mchungaji Peter Mitimingi.

Mada zilizowasilishwa katika kongamano hilo ni pamoja na ulimwengu wa vijana na zinaa, madhara ya vijana kujichua (punyeto), madhara ya vijana kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa pamoja na uthamani wa ubikira kwa vijana, mada ambazo zilipokelewa vyema na vijana hao ambao wengi wao walimpa Yesu maisha yao mara baada ya kupewa nafasi hiyo.

Aidha pia katika kongamano hilo ambalo halikuwa na kiingilio, mwanadada Martha Baraka aliweza kuwabariki wengi kwa uimbaji wake kikiwemo kibao chake cha 'Yesu jina kubwa' ikiwa pia huduma ya chakula ilitolewa kwa wahudhuriaji wa kongamano hilo. VHM wamekuwa wakijihusisha na injili maeneo yasiyifikiwa ama kuwa na matatizo ya nguvu za giza, ambapo shuhuda zimeendelea kumiminika popote huduma hiyo inapotia mguu kutokana na watu wengi kuponywa na kufunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali.
Vijana wakikusanyika tayari kwa kongamano ukumbi wa St. Mary Forest Mbeya. 
Nafasi ndani zilijaa kabisa hivyo vijana wenginekuamua kukaa nje.
Acha kabisa, sifa zikivumishwa na mwanadada Martha Baraka huku tabasamu kuubwa kutoka kwa mchungaji Mitimingi.
Mchungaji Mitimingi akionyesha kwamba wamo kwenye kumsifu Mungu, akicheza sambamba na Martha Baraka.
Ulikuwa wakati mzuri cha mafundisho.

Vijana wakifuatilia kongamano.
Mavuno ya kutosha yalipataikana kwa vijana kumrudia Kristo.
Mchungaji Mitimingi akizungumza na vijana waliopita mbele kumkabidhi Kristo maisha yao.
Ilikuwa wakati wa kushibisha matumbo kwa chakula cha kimwili.
Washiriki wakiwa katika foleni ya chakula.
Mchungaji Mitimingi akiongozwa na Askofu Msolo kwenda kula chakula.

Comments