KWA NENO LA MUNGU,NITAZISHUSHA NYAVU * sehemu ya kwanza *

Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


" Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.

Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;
wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama. " Luka 5:5-7

Nakusalimu ndugu mpendwa katika jina takatifu la Yesu Kristo;
BWANA YESU ASIFIWE...

Bwana Yesu Kristo,yupo hapa saa hii;Roho mtakatifu akusaidie sasa kukufundisha fundisho hili la imani siku ya leo,nami ni maombi yangu kwa Mungu Baba wa utukufu wote,akufundishe kwa lugha nyepesi ya kueleweka siku ya leo ukapate kuelewa kwa namna ya utofauti kabisa.

Ninaposema " kwa neno la Mungu,nitazishusha nyavu " nina maana hii;
*Kwa msaada na nguvu za neno la Mungu,nitafanya kazi na kufanikiwa kwa viwango vya hali ya juu mno.

Mafanikio halisi yamefichwa katika neno la Mungu. Nje ya hapo hakuna kustawi kiroho wala kimwili.
Neno " nyavu " huwakilisha kitendea kazi.

Sasa,
Huwezi kufanikiwa pasipokuwa na nyavu.
Katika andiko hilo hapo juu,kama Simoni asinge'likuwa na nyavu,basi asinge'weza kuvua samaki hata kama neno lilitamkwa,neno liliungana na nyavu,ndiposa samaki wakavuliwa.

Kiimani,nyavu ni CHOMBO CHA KUPOKELEA.
*Kanuni ya kupokea mbaraka ni lazima uwe na chombo cha kupokelea.
Maana;
Mbaraka hauji juu ya kichwa chako,au katika tumbo lako,bali mbaraka huja katika KAZI YA MIKONO YAKO.
Andiko husema hivi;

" Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. " Kumbukumbu 28:5

Kubarikiwa kwa kapu lako,na chombo cha kukandia unga ni kubarikiwa kwa kazi ya mkono wako. Kwa lugha nyingine ni kwamba,ikiwa kama huna " kapu " au " chombo " basi husitegemee mbaraka.

Simoni na wenzake walikuwa na chombo cha kupokelea muujiza wao yaani nyavu.
Walichokuwa wakihitaji ni NENO la MUNGU liletalo imani hata kuweza kutumia nyavu ipasavyo.

Nami nazungumza na wewe,ukihitaji kuona mafanikio halisi ni lazima uwe na " nyavu" kama chombo cha kupokelea,na pili ni lazima uwe na NENO LA MUNGU KWA WINGI NDANI YAKO.
Ipo shida katika siku ya leo;
Watu wengi uhitaji kupata mafanikio ya kiroho na ya kiuchumi ali wakiwa hawana NENO LA MUNGU pia kukosa NYAVU.

Watu hukazania " MUNGU nibariki,MUNGU nibariki,MUNGU nibariki..." na hawabarikiwi ngo'! Kwa sababu ya kukosa maharifa,
Tazama;
Wakristo wa leo,wale wapendwa;
Utakuta kweli wameokoka,lakini hawana chombo chochote cha kuzalisha mafanikio, yaani " nyavu "

Utakuta mtu amekosa hata kuuza genge la nyanya au vitunguu,au hata kuuza karanga N.K lakini mtu huyo huyo akizidi kuomba Mungu ambariki pesa, sasa swali langu;
Hizo pesa zitakujaje,pasipo NYAVU ?

Mfano mdogo tu;
Siku moja nilitembelea mjini posta-Dar es salaam,ilikuwa majira ya asubuhi asubuhi hivi,niliposhuka tu katika dalala,pale Posta mpya,gafla wakina mama kama watatu hivi,wakanifuata wakiwa wameshika vikombe vya chai na pembeni kulikuwa na vitafunwa mbali mbali yaani maandazi,vitumbua,samaki N.K

Wakina mama hawa kila mmoja aliniambia " Karibu kaka uje ukae hapa,kuna chai ya maziwa,ya rangi,shika kikope hiki,shika sasa,chukua,njoo..."
Nami nikajikuta nikachukua kikombe cha mama mmoja na kuanza kunywa chai kwake.

Wakina mama hawa walikuwa wana NYAVU wakitega.

Sasa,watu hawa ni watu wa mataifa lakini wana akili ya KUTEGA NYAVU zao hata kupata pesa,na ukweli wanafanikiwa kwa kupata pesa.
Je si zaidi sana kwa mtu aliyeokoka aliyetega nyavu zake?
Maana mtu aliyeokoka,Mungu huwa upande wake.

Walokole wa leo,hudhania kwamba Mungu atawashushia pesa pasipo NYAVU!
Mimi ninakuambia hakuna muujiza wa namna hiyo,
Ukitaka kufanikiwa,basi huna budi kulijaza neno la Mungu kwanza,kisha uwe na mitego au vyombo au NYAVU ya kuvulia.

Ok,
Andiko tulilolisoma hapo juu,ukisoma kuanzia mstari wa kwanza,hadi ule wa kumi na moja ( Luka 5:1-11)tunaona makutano wakimsonga Bwana Yesu wakisikiliza neno.
Biblia haikusema kwamba makutano walipomsonga Bwana Yesu;walimsonga kwa ajili ya kuombewa.
Pia Biblia haikutuambia ya kwamba walimsonga kwa ajili ya kuwekewa mikono kwa kutuoa mapepo au la?

Bali neno linasema wazi kabisa ya kwamba makutano walimsonga kulisikiliza neno la Mungu. Hii inatupa picha kwamba;makutano walikuwa na shauku ya kuisikia sauti ya Mungu. Au,makutano walikuwa na njaa na kiu ya kuisikia KWELI YA MUNGU.

Ali Bwana Yesu akijua shauku ya makutano,akaamua kuketi chomboni mwa Simoni, akamtaka akipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano ali chomboni.
Kile alichokuwa akiwafundisha ilikuwa ni IMANI,maana baada tu ya kuwafundisha kwa theory akawataka wafanye practical,yaani ;
*Imani huja kwa kusikia neno la Kristo,( Warumi 10:17). Na imani ili iwe imani ni lazima matendo yafanyike,

"Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake." Yakobo 2:17

Ndiposa,Bwana Yesu alipomaliza kuwafundisha,alimuhitaji Simoni atweke mpaka kilindini akavue samaki. Hapo Bwana Yesu,aliwahitaji wakina Simoni WATENDE baada ya kusikia.
Biblia inatuambia maana ya imani kwamba;

" Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. " Waebrania 11:1
Simoni hakuona samaki,bali Yesu aliona samaki ndio maana akamtaka Simoni akavue samaki,
* Imani ni kuona visivyoonekana kwa macho ya damu na nyama,bali vionekanavyo kwa macho ya rohoni.

Bwana Yesu asifiwe...
Jina la Bwana Yesu lisifiwe sana....

Mara nyingi katika maisha yetu,tumekuwa ni watu tusioona mambo ya rohoni,tukitalaji kuona kwa macho ya damu na nyama.
Shida kubwa iliyopo kanisani leo,ni kupungukiwa kwa imani,hata kushindwa kumpendeza Mungu,maana pasipo imani haiwezekani kumpendeza ( Waebrania 11:6)

Sasa angalia;
Simoni ajibuvyo pale alipoambiwa atweke mpaka kilindini,akajibu;
" Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. " Luka 5:5

Kwanza kabisa nampenda Simoni,maana alitambua ya kwamba Yesu Kristo ni Bwana mkubwa ingawa yeye Simoni alikuwa ni mdhambi...

ITAENDELEA...

* Kwa huduma ya maombi na maombezi,usisite kunipigia simu kama vile wanipigiavyo wengine. Leo kuwa mmoja wao,piga;
0655111149.

Usikose utamu wa fundisho hili!

UBARIKIWE.

Comments