KWA NENO LA MUNGU,NITAZISHUSHA NYAVU.*sehemu ya pili.*

Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


" Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. " Luka 5:5

Kwanza kabisa nampenda Simoni,maana alitambua ya kwamba Yesu Kristo ni Bwana mkubwa,ingawa yeye Simoni alikuwa ni mdhambi kipindi hicho Yesu alipowatokea.

Kulikuwa na udhihilisho wa Mungu ndani ya Yesu Kristo,uliongara hadi kwa nje hata kutambulikana ya kwamba ni " Bwana mkubwa " ( Sababu Yeye mwenyewe Kristo ni Mungu aliyeuvaa ubinadamu kisha azaliwe chini ya sheria kusudi la kukomboa wote walio chini ya sheria) hata Simoni alipomuona,baada ya kusikia,akasema " Bwana mkubwa". Sio jambo rahisi kumtambua mtu asiyejitambulisha kwako,Lakini kile kitu alichokibeba Yesu,ndicho kilichomsukuma Simoni kutambua udhihilisho huo.

Neno " Bwana mkubwa " katika biblia ya kiingereza ya amplified bible,limeandikwa "Master," ikiwa na maana kwamba Yesu Kristo ni zaidi ya mwalimu wa kawaida.
Bwana Yesu,alikuwa akiwafundisha wakina Simoni, maana Yeye ni mwalimu wa walimu.

New king james version,( NKJV) ameandika vivyo hivyo;
Tunasoma;
" But Simon answered and said to Him, “Master, we have toiled all night and caught nothing; nevertheless at Your word I will let down the net.” Luke 5:5

Bwana Yesu asifiwe....
Nasema; Bwana Yesu asifiwe sana...
Haleluyaa...

Ikumbukwe ya kuwa;
* Mafanikio halisi yamefichwa katika neno la Bwana Mungu.
Ndani ya neno la Bwana ndipo mahali ambapo mafanikio yalipo.
Kwasababu,utendaji kazi wa Roho mtakatifu utegemea NENO LA MUNGU.

Kwa lugha nyepesi,ninaweza kukuambia ;
* Roho mtakatifu hutenda kazi ndani ya neno lake,yaani neno la Mungu.
Tazama hapa mpendwa wangu katika Kristo Yesu,tunasoma;

"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. " Mwanzo 1:1-2

Biblia inatuambia ya kwamba nchi ilikuwa ukiwa,alafu sio ukiwa peke yake bali pia tupu,tena na giza lilikuwa juu ya uso wa maji,.Roho wa Mungu akatulia juu ya uso wa maji.

Biblia hakusema ni muda gani ambao Roho wa Mungu aliutumia kutulia juu ya uso wa maji. Hatuelezwi kuwa ilikuwa ni siku ngapi,au miezi mingapi,au miaka mingapi,au hata karne ngapi, ambazo Roho mtakatifu alitulia juu ya uso wa maji. Lakini jambo moja ninalolijua ni kwamba,HAKIKUTOKEA CHOCHOTE KILE.
Mpaka mstari wa tatu ( Mwanzo 1:3) mahali ambapo tunasoma;

" Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru."

Ndiposa Roho mtakatifu akatenda ndani ya lile neno. Roho mtakatifu alilisubiri neno la Mungu,ili atende.Ndio maana nakuambia kwamba Roho mtakatifu hutenda ndani ya neno lake.

Umenipata hapo?

Bwana Yesu asifiwee...
Haleluya...,nasema Haleluya...

Nami ninakuambia,Hakika kwa neno la Kristo utazishusha nyavu,maana ndani ya neno,upo utendaji kazi wa Roho mtakatifu.
Nje ya Neno la Mungu,hakuna utendaji kazi wa Roho mtakatifu.

Andiko hilo hapo juu ( Luka 5:5) Simoni alipokiri ya kwamba kwa neno la Kristo atazishusha nyavu,alimruhusu Roho mtakatifu aingie kazini ili lile neno likapate kuwa dhahili. Lakini pia tazama namna ambavyo muujiza huu wa Roho mtakatifu ndani ya neno la Kristo ulivyotimia.
Neno lilipoachiliwa,Roho mtakatifu akaliwezesha,Simoni naye akatafuta chombo cha kupokelea muujiza huo wa kuvua samaki wasiokuwa na idadi.

" Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, " Luka 5:4

Chombo chake Simoni cha muujiza, kilikuwa ni NYAVU,ndiposa tunaona ukamilifu wa muujiza huo ukitokea.

Roho mtakatifu alikuwa na uwezo wa kuwatoa samaki wote wa baharini kipindi hicho cha kina Simoni,kisha ampe Simoni.Lakini hiyo siyo kanuni ya Mungu maana Roho mtakatifu alimuhitaji Simoni awe na NYAVU kama chombo kwa kazi ya mkono wake. Mungu wetu tunayemtumikia ni Mungu wa utaratibu,anapoachilia neno kwako kupitia mtumishi wake,hapo anakutegemea na wewe uwe na NYAVU kama chombo cha kupokea huo mbaraka kwa kazi ya mkono wako,na hiyo ndio kanuni ya ki-Mungu.
Huna chombo,husitegemee mbaraka!

Chombo ni nyavu,
Nyavu ni kazi ya mikono yako.

Mtumishi anapotupa neno kwako,ili neno lile lizae ni lazima uwe na NYAVU,yaani uwe na chombo kazi ya mkono wako.

Mfano;
Nyavu za mwanafunzi ni masomo. Ili ufaulu inakuhitaji ukalisikie neno la Bwana kwa usahihi wake,na maombi,kisha ushushe nyavu/ usome kwa bidii. Hapo utamuona Mungu akitenda ndani yako,la sivyo maombi peke yake hayafai.
Maana;
Haiwezekani ukaja kwangu,kisha nikakuombea ufaulu kwa viwango vya juu,alafu wewe mwenyewe usimaanishe ukawa husomi kwa bidii,kwamba unategemea maombi niliyoyafanya kwako yakabadili mtihani uliotungwa. Au maombi niliyofanya yakabadili majibu uliyojaza katika mtihani.

Usisahau hii;
Ukihitaji kufanikiwa kiroho na kiuchumi basi,lijaze neno la Kristo ndani yako baada ya kuokoka,kisha uchukue hatua madhubuti ya KUSHUSHA NYAVU kwa neno la Mungu.

Sasa;
Unisikilize mpendwa;
Ninakuambia ya kwamba;mafanikio halisi yamefichwa katika neno la Bwana Mungu.

Yawezekana umeshafanya kazi sana pasipo kuona mafanikio,
Yawezekana kabisa umeangaika vya kutosha kutafuta kazi,siku nyingi lakini umekosa.
Yawezekana umetafuta mchumba kwa muda mrefu hadi umri wako umekwenda sana,pasipo hata kuona mafanikio.
Au yawezekana upo ndani ya ndoa,lakini ndoa yenyewe ni ndoa ndoano yaani hakuna hata AMANI kwa muda mrefu bila mafanikio.

Au;
Umetafuta mtoto katika ndoa yako kwa muda mrefu,lakini hukupata majibu,kama vile akina Simoni walivyofanya kazi USIKU KUCHA BILA MAFANIKIO KWA KUTEGEMEA AKILI ZAO.
Leo;
Neno linasema " kwa neno lako Mungu,nitazishusha nyavu- na kufanikiwa"

Sikia;
Huitaji dawa yoyote ile,bali unahitaji NENO LA MUNGU kutatua matatizo yote hayo,na kufanikiwa.

Siku hizi za leo,wapo watu waliokosa matumaini kwa kufanya kazi usiku kucha bila mafanikio. Wengine waliangaika vya kutosha kwa madaktari juu ya afya zao,lakini hawakupata mafanikio ya kuzikomboa afya zao. Tazama sasa baadhi ya watu hao,walipokuja kwa Yesu,wakaokoka.
Kisha wakaliangalia neno la Bwana,wakazitupa nyavu zao,wakafanikiwa kiroho hadi kiuchumi pia.

Haleluya...
Sijui kama yanakuelea haya nikuambiayo siku ya leo,muda huu;

Tazama;
Simoni alikuwa akifanya kazi yake ya uvuvi kwa kutegemea UJUZI /Skills & Experience ,lakini biblia inatuambia hata kwa uzoefu na ujuzi wake ulifikia kikomo mahali ambapo hakupata kitu. Upo ukomo wa ujuzi wako ulio nao,Lakini neno la Mungu halina kikomo.
Suala sio ujuzi wala uzoefu,bali suala ni KULIANGALIA NENO LA KRISTO,LINASEMAJE.

Siku zote mazingira husema kinyume na matarajio yako uliyoyapanga,kila unachojaribu kupanga,hakipangiki. Na hii hali huwa ni kwa sababu unatumia AKILI zako na wala si NENO la KRISTO linasemaje.
Hivi,ngoja nikuulize swali,
Unafikiri Simoni hange'weza kupata mafanikio yote ya kuvua samaki wengi namna ile,pasipo neno la Kristo?

Kama jibu ni hapana,kwamba asinge'weza. Basi vivyo hivyo na kwako,huwezi kufanikiwa kwa viwango vya juu nje ya neno la Mungu...

ITAENDELEA...

*Naomba niombe na wewe uliyesoma ujumbe huu. Ndani yangu najisikia niombe na wewe,wala usisite maana ni Bwana Yesu Kristo ndie atakuhudumia.
Unipigie sasa kwa namba yangu hii;
0655111149.

* Usikose fundisho hili mahali hapa hapa.

UBARIKIWE.

Comments