
Walidai kuwa wakristo wanawakanganya waislamu walio wengi na hilo laweza kuhatarisha usalama wa taifa.
Uamuzi huo, ni mojawapo ya mikondo ya mwisho ya kesi za kisheria za kanisa katoliki zilizochukua muda wa miaka saba na ambao umesababisha mashambulizi katika makanisa, majumba ya maombi ya waislamu na pia hekalu la wasikh katika mwaka wa 2010.
Wakristo na wasikh wanadai kuwa wamekuwa wakimwita Mungu, Allah katika lugha za kiMalay na Sansrit kwa muda mrefu sana.
Mahakama nayo imeshikilia uamuzi wao wa awali kuwa jina hilo halifai kuingizwa katika ukristo.
Viongozi wa kanisa wanaogopa kuwa uamuzi huo utasababisha kizingiti kwa washiriki wake milioni mbili. Mgongano huo kuhusu neno hilo moja umedhihirisha jinsi nchi hiyo yenye dini na kabila tofauti tofauti lilivyogawanyika.
Wanaharakati
wa kiislamu wamekua wakishabikia uamuzi huo nje ya majumba ya
koti,wengi wao wanaamini kuwa wakristo wanamwita Mungu, Allah, kama njia
ya kuwavuta waislamu wajiunge na ukristo, shutma ambazo wakristo
wamekana.
Mwanasheria mmoja anayewakilisha kanisa katholiki anashauri kuwa bado wanaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama.
..........XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX......
Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani; mkituombea na sisi pia, kwamba MUNGU atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya KRISTO, ambayo kwa ajili yake nimefungwa, ili niidhihirishe, kama inipasavyo kunena. Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.-Wakolosai 4:2-6.
Wajue ya kuwa wewe uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako uliye juu ya nchi yote-Zaburi 83:18
Kisha MUNGU akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama MUNGU Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.-Kutoka 6:2-3.
YESU KRISTO ndio siri ya MUNGU, Ukitaka kumjua MUNGU basi mpokee BWANA YESU.- Wakolosai 2:2b
JEHOVAH ADONAI akubariki sana na nakutakia siku njema.
Comments