 |
Joyce Ombeni pamoja na Christina Matai wakiimba msibani hapo jana. |
Mazishi ya aliyekuwa mwimbaji wa muziki wa injili nchini Debora John
Said ambaye pia alikuwa mama mchungaji, yanatarajiwa kufanyika majira ya
saa nane mchana wa leo katika makaburi ya Makuburi jeshini jijini Dar
es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo GK imezipata, ni kwamba ibada ya mazishi
inatarajiwa kuanza majira ya saa nne asubuhi nyumbani kwa marehemu kisha
msafara wa kuelekea kwenye kuupumzisha mwili unatarajiwa kuwa majira ya
saa saba mchana. Toka kutokea kwa msiba huo, waimbaji mbalimbali
wamefika msibani hapo kutoa faraja kwa nyimbo na wengine kufikia hatua
ya kuzimia kutokana na huzuni ya kuondokewa na mwimbaji mwenzao.
Kati ya waimbaji walioimba siku ya jana ni pamoja na mwanamama Christina Matai, Victor Aron,
 |
Marehemu Debora John Saidi. |
Sarah Mvungi, Sifa John ambaye alizimia wakati akiimba kutokana na
majonzi, wengine ni Joyce Ombeni, Mc Joshua Makondeko ambaye alikuwa
karibu na marehemu hata wakati anaumwa kwa kumtembelea hospitalini
pamoja na nyumbani akiongozana na waimbaji wenzake, lakini pia wanakwaya
kutoka kanisa alilokuwa akiabudu marehemu wengi wao walizimia wakati
wakiimba wimbo maalumu kwa mama mchungaji wao ambaye hawatamuona tena.
Chini ni moja ya uhuhuda kutoka kwa mwimbaji Rungu la Yesu kama
alivyouandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kumuelezea marehemu jinsi
alivyofanyika baraka katika maisha yake ya huduma.
NAKUMBUKA MARA YA MWISHO ALINIPIGIA SIMU
NIENDE KWENYE HUDUMA YAO AMBAYO NI BRANCH YA MAISHA YA USHINDI
VINGUNGUTI KWAMNYAMANI PALE SOKONI,NIKAMSTUA BASHANDO TUKAENDA KUWASHA
MOTO,NASIKITIKA KWASABABU MARA NYINGI AMEKUWA MAMA ALIYEKUWA AKINITIA
MOYO SANA NA KUNIAMBIA MWANANGU RUNGU SONGA MBELE,TUMPATE WAPI MAMA
KAMA HUYU TENA MAMA ANAYEJUA KUWALEA WATU KANISANI KWAKE KILA MUIMBAJI
ANAKARIBISHWA BILA KUJALI UNAJULIKANA KIASI GANI,SIUMII KWASABABU
AMEKUFA MAANA BIBLIA INASEMA HERI WAFU WAFAO KTK BWANA,HILA NAUMIA
KWASABABU ALIKUWA MAMA MWENYE UPENDO NA KUMJALI KILA MTU HIVI TUTAMPATA
WAPI MAMA KAMA HUYU TENA? NAHISI MOYO WANGU UMEKUFA GANZI NA KUFIKA
MBALI ZAIDI KWA NINI MUNGU ASINGE MWACHA KIDOGO LKN BWANA AMETOA BWANA
AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE,MIAKA SITA ILIYOPITA MAMAYETU DEBORA
JOHN SAIDI NA NA MCHUNGAJI JOHN SAIDI WALITUOMBEA MAOMBI MAZITO SANA
PALE KANISANI KWAKE VINGUNGUTI BAADA YA KUFANYA TAMASHA LA GOSPEL HIP
HOP,MAOMBI YALIKUWA HIVI"UWAINUE,UWAPE KIBARI WAFANIKISHE KIRO NA
KIMWILI,WAPE MAGARI YAO WAPE NYUMBA ZAO NA WAPE HATA VIWANJA VYA
KUJENGA" BAADA YA MAOMBI HAYO TUKIWA TUNAMTUMIKIA MUNGU MILANGO IKAANZA
KUFUNGUKA WENGINE KWELI WAKAPATA MAGARI,WENGINE SASA WAMEJENGA,WENGINE
SASA WANAVIWANJA NA MASHAMBA WENGINE SASA NI WATU WA KUBWA
SANA...NIISHIE HAPO SINA CHA KUSEMA TUZIDI KUMWOMBEA BABA YETU MCHUNGAJI
JOHN SAIDI NA FAMILIA NZIMA MUNGU AWATIE NGUVU KWENYE KIPINDI KIGUMU
HIKI...JUMATATU SAA NNE ASUBUHI KATIKA KANISA LA USHINDI LILOPO MABIBO
EXTENAL TUTAKUWA NAIBADA YA MWISHO YA ALIYEKUWA MPENDWA WETU,LKN MSIMBA
UNAENDELEA PALE NYUMBANI KWAO MABIBO HOSTEL UKIFIKA TU PALE UWEZI
KUPOTEA...TIMU NZIMA YA YESU OKOA MITAA TUTAKUWA PALE NA WEWE POPOTE
ULIPO SOGEA PALE...YESU OKOA MITAA- KILA KONA YA MTAA....YOM.
BAADHI YA PICHA KUTOKA MSIBANI WAIMBAJI WAKIIMBA HAPO JANA
 |
Joyce pamoja na Christina Matai wakiwa msibani kutoa faraja. |
 |
Sifa John akimsifu Mungu msibani hapo. |
 |
Sifa John akimsifu Mungu. |
 |
Makondeko, Matai, Mvungi pamoja na Ombeni wakiwa pamoja.
|
 |
Mwinjilisti Sarah Mvungi akimtukuza Mungu. |
 |
Sifa John akiwa amezimia msibani hapo. |
 |
Victor Aron akiimba huku Addo November na waimbaji wengine wakiwa sambamba naye. |
 |
Joshua Makondeko akimsifu Mungu msibani hapo. |
 |
Mc Joshua Makondeko akimsifu Mungu. |
 |
Christina na Joyce Ombeni wakiimba. |
 |
Christina Matai akimsifu Mungu.source:Gospel kitaa |
|
Comments