MIMI SIO KAMA WALE( 2)

Na Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima.
Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe
 




Danieli3: 1 Nebukadreza, mfalme, alifanya sanamu ya  dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli.
2 Ndipo Nebukadreza akatuma watu kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha.
3 Ndipo maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, wakakusanyika ili kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha; wakasimama mbele ya ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha.
4 Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele akisema, Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi,
5 wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha.
6 Na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao.
7 Basi wakati huo, watu wa kabila zote walipoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, watu wote na mataifa na lugha wakaanguka, wakaiabudu ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha.
8 Basi baadhi ya Wakaldayo wakakaribia, wakaleta mashitaka juu ya Wayahudi.
9 Wakajibu, wakamwambia mfalme Nebukadreza, Ee mfalme, uishi milele.
10 Wewe, Ee mfalme, ulitoa amri ya kwamba kila mtu atakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, ni lazima aanguke na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu;
11 na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa katika tanuru ya moto uwakao.
12 Wako Wayahudi kadha wa kadha uliowaweka juu ya mambo ya wilaya ya Babeli, yaani, Shadraka, na Meshaki, na Abednego; watu hawa, Ee mfalme, hawakukujali wewe; hawaitumikii miungu yako, wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.
13 Basi Nebukadreza akatoa amri kwa hasira na ghadhabu, waletwe hao Shadraka, na Meshaki, na Abednego. Basi wakawaleta watu hao mbele ya mfalme.
14 Nebukadreza akajibu, akawaambia, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, je! Ni kwa makusudi hata hammtumikii mungu wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha?
15 Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu?
16 Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili.
17 Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme.
(Danieli6:1-28)  1 Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote;
2 na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danielii alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara.
3 Basi Danielii huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.
4 Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danielii kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.
5 Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danielii huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake.
6 Basi wale mawaziri na maamiri wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi, Mfalme Dario, uishi milele.
7 Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba.
8 Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika.
9 Basi mfalme Dario akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku.
10 Hata Danielii, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
11 Basi watu hao wakakusanyika pamoja, wakamwona Danielii akiomba dua, na kusihi mbele za Mungu wake.
12 Ndipo wakakaribia, wakasema mbele ya mfalme katika habari ya ile marufuku ya mfalme; Je! Hukuitia sahihi ile marufuku, ya kwamba kila mtu atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme, atatupwa katika tundu la simba? Mfalme akajibu, akasema, Neno hili ni kweli, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi isiyoweza kubadilika.
13 Basi wakajibu, wakasema mbele ya mfalme, Yule Danielii, aliye mmoja wa wana wa wale waliohamishwa wa Yuda, hakujali wewe, Ee mfalme, wala ile marufuku uliyoitia sahihi, bali aomba dua mara tatu kila siku.
14 Basi mfalme aliposikia maneno haya alikasirika sana, akakaza moyo wake ili kumponya Danielii; akajitaabisha kumwokoa hata jua likachwa.
15 Ndipo watu wale wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia mfalme, Ee mfalme, ujue ya kuwa ni sheria ya Wamedi na Waajemi, lisibadilike neno lo lote lililo marufuku, wala amri yo yote iliyowekwa na mfalme.
16 Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danielii, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danielii, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.
17 Likaletwa jiwe, likawekwa mdomoni mwa lile tundu; naye mfalme akalitia muhuri kwa muhuri yake mwenyewe, na kwa muhuri ya wakuu wake, lisibadilike neno lo lote katika habari za Danielii.
18 Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa.
19 Asubuhi mfalme akaondoka mapema, akaenda kwa haraka mpaka penye lile tundu la simba.
20 Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danielii kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danielii, Ee Danielii, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa?
21 Ndipo Danielii akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele.
Hao walikuwa ni wafalme wanchi ingekuwa leo ni Raisi nchi na hawa wanatoka katika ufamle ule ule na kwenye falme hizi hizi Nebukadreza na dairo ikatokea siku moja jambo likatokea la ajabu na mfalme Nebukadreza akatoa tamko la ajabu iletwe sanamu yake ya dhahabu  na kutakuwa na dhifa ya taifa na mawaziri, madiwani, wakuu wa mkoa na kutakuwa na mziki wa kinubi,santuri, na zeze na utakapo sikika watu wote wanatakiwa waiabudu ile sanamu na atakaye kaidi atatupwa katika moto na hii ilikuwa inawalenga watu fulani na mtu huwa anafanya hayo pale anapokuwa katika utawala wake ndio maana anatumia uzoefu ule kuwaondoa na hawa pasipokujua kuwa wao sio kama wale na uzoefu wao utakwama, sasa kulikuwa kuna watu watatu Shadraka,  Meshaki, na Abednego ambao walikuwa hawayafuati masharti yao.
Inawezekana tatizo ulilo nalo limetengenezwa ili wewe uporomoke useme hii ni kazi ya Mungu useme Bwana alitoa na Bwana ametwaa, unatakiwa  ukatae kwa jina la Yesu. Na yapo mambo mengi yanatengenezwa juu yako na hao wanao yatengeneze wanadhani hapa ‘hatatoka tumemkamata’ lakini hawajui yakuwa “mimi sio kama wale” na namna ya kushinda vita ni kupita katikati yao na jaribu likija hutakiwi ulikwepe unatakiwa usimame mbele yake halafu unasema napita katikati yao.
Wakakusanyika watu wakadondoka chini halafu kina shadraka, meshaki, na Abednego wakasimama  wakaonekana wamesimama na baada ya muda mfalme akapewa taarifa kwamba kuna viyahudi havikusujudu na mfalme akaamuru waletwe kwake na akawaambia ni kwamakusudi kweli ni nadhani bahati mbaya lakini sasa naomba irudiwe tena zeze na vinubi ili msujudu lakini wakakataa na mfalme akawaambia nawatupa kwenye moto lakini wakamjibu tuko tayari kuingia kwenye moto na Mungu wetu atatuokoa na Biblia inasema mfalme akamuru moto uwashwe marasaba zaidi kuliko ilivyokuwa desturi yake, inawezekana kuna watu wanakuwashiwa moto kwenye maisha yao ili wakuteketeze lakini wewe sio kama wale. Basi mfalme akaamuru wafungwe, na shetani akiamua kukufunga anakufunga vilevile ulivyo na gari lako na nyumba yako, basi wao wanajua moto ulishawaunguza wengine iwe wao ambao wamewashiwa mara saba zaidi pasipo kujua wao sio kama wale sema Mimi sio kama wale. Basi mfalme akasema watupiwe kwenye moto na wale walio wabeba wakatekea wao kwanza hata kabla hawajaingia kwenye moto.
Mwone yuda alimsaliti Yesu lakini yeye alienda kujinyonga kabla Yesu hajafa. Biblia inasema aliyekupandia ubaya na yeye ubaya hautatoka nyumbani mwake”. Sasa walipoingia kwenye moto wakaonekana wanne na mmoja kama mwana wa Mungu na vifungo vyao vimefunguka na mfalme akawaita na watu wote wakaogopa na kutukuza mbele ya Mungu wa shdraka, meshak, na abernego. Huyu alikuwa ni mfalme Nebukadreza.
Mfalme Dairo yeye aliweka amri ya siku 30 mtu atakaye abudu Mungu mwingine atatupwa kwenye tundu la simba lakini aliyekuwa analengwa ni Danieli na danieli alikuwa anaabudu kwa kujificha na baadae akaamua kufungua madirisha na milango ili asikike na wale waliokuwa wamepanga kwaajili ya kumuondoa na kumwangamiza walimsikia na kwenda kumshitakia kwa mfalme na mfalme akaamuru atupwe kwenye tundi la simba. Zamani simba waliwekwa kwenye mashimo marefu na waliohukumiwa kifo walikuwa wanatupwa kwenye tundu hilo na simba walikuwa wanakula nyama za watu tu na safari hii wakaamuru kubadilisha asiye mwabudu mfalme atupwe huku ndipo wakamtupa danieli na mfalme akatia mhuri kwenye jiwe hilo. Ilikuwa ni kwasababu ya wivu tu na mfalme baadae alifahamu kumbe aliye lengwa ni danieli na akaamua kujaribu kumuokoa Daniel pale akijua kwamba kumbe ishu hii ni kwaajili ya mtu tu. kila mbegu iwe ni mbegu iwe ya harage,au yeyote ina mti wewe hautakatizwa hadi utoe mti kwa jina la Yesu, ubuyu una mti ndani na ukichukua ubuyu ukaunyonya ukaweka mfukoni mbegu yake jua kwamba una mti wa ubuyu ndani ya mfuko na ukienda kuupanda unakuwa mti mkubwa. Kila mtu unaye mwona ana makusudi ya kufanikiwa aliyopewa na Bwana. Watu wengi huwa wanawaza kufanikiwa ni kuolewa, kujenga nk, hapana ni lile kusudi ulilowekewa ndani yako ulipokuja duniani na lile kusudi likitimia unaitwa umefanikiwa na mtu anapofariki bila kufanya kusudi lake anaitwa hajafanikiwa na kusudi haliwezi kuzuiwa na mwandamu na Ufufuo na uzima kusudi letu ni kuigeuza Tanzania igeuke iwe Ufalme wa mwana kondoo na hakuna atakaye weza kugeuza kusudi hili. Na Mungu amewaweka watu kwenye maisha yao labda kutokuwapa mali nyingi kwasababu anajua kwa sampuli ya moyo huu huyu mtu ataniacha nikimpa Gari mapema na Mungu anaruhusu jambo fulani likupate ili akutengeneze na kwa kadiri unavyo barikiwa unatakiwa usonge mbele.
 Sisi tumeitwa kuihubiri injili hatujaitwa kuongea maneno sisi sio kama wale sisi ni kizazi tofauti kuna watu wenye nia ya kukurudisha  chini jua ya kwamba wewe sio kama wale waliowarudisha chini. Anaye kuvuta kukushusha chini lazima yeye awe chini kwanza lakini wewe hauetaenda chini kwa jina la Yesu, sema nakataa kurudishwa chini na wanadamu, wachawi ,wasoma nyota, mashetani nakataa kurudishwa chini kwa jina la Yesu.
Kuna baadi ya watu wamewekewa magonjwa na watu ili wanataka wewe urudi chini na kama jambo hulifahamu lipime kwa wakati na muda, na mambo yote ya shetani yana muda mfupi tu kila kilichotengenezwa na wanadamu kina mwisho wake hatakama haupendwi na unapigwa vita na ndugu au rafiki zako au wafanyakazi wako. Biblia imeandikwa tutamiliki milango ya adui zetu, Mungu ni wa ajabu Yule mtu unaye mchukia ndiye anamweka mlangoni na anaweza kuficha muujiza wako ndani ya mtu unaye mchukia. Modekai yupo mlangoni waziri mkuu Hamani anapita ameamuru watu wote wainame anapopita. Na mfalme alikuwa ana mungu wake na alikua anaabudu mizimu kila mwaka miezi mitatu alikuwa anaabuddu mwenyewe bila mkewe wala mtu yeyote na haman akaongea akaandika waraka wa kuharibu akamwambia mfalme kuna kabila moja hapa naomba utoe amri wauliwe na akaweka ule muda mfalme alikuwa anaabudu mizimu na mfalme akampa Yule mbaya na pete yake akaandika siku Fulani (wakati mfalme alikuwa anaabudu mizimu yakee) akaitoa ikasambazwa ili wayahudi wauwawe. Basi haman akaachiwa ikulu na wayahudi walipousoma waraka wa kifo,  ’’ nakutaarifu kila silaha itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa, usifurahi ee adui yangu ninapo anguka nitainuka tena, mabaya hayata nitapata tena’’. Wayahudi walipo uona waraka wakamlilia mfalme ambaye hakuwepo imekuwaje lakini nakutaarifu kuachwa na watu sio kuachwa na Mungu usiogope wakikuambia naacha kukusaidia mwambie acha usiogope Mungu tunaye mtumikia anaweza kutuwezesha.
Waraka ukaandaliwa na anayetaka kukuua atakufa kabla yako, Baadae kumbe mfalme huyu bila kujua kumbe mke wake yeye ni myahudi na modekai naye alikuwa ni myahudi alikwenda kumwambia Esta unataarifa waraka wa kuwaua wayahudi na esta akasema mfalme amekwisha kuingia kuabudu na kwa desturi hairuhusiwi kuingia hukoesta akamwambia siwezi kuwasaidia na Modekai akamwambia usipowaokoa wayahudi kwa njia hii Mungu atawasaidia kwa njia nyingine na wewe pia usiposaidiwa na mtu umtegemeaye, Mungu atakusaidia na mtu mwingine. Baadae esta akawaambia fungeni siku tatu na mimi nitaingia kwa mfalme kinyume cha sheria na wakati huo amri inaendelea kuwepo na inawezekana wewe kuna mpango umewekwa juu yako kukuangamiza na wewe huujui unatakiwa useme mimi sio kama wale. Modekai akamwambia esta usipotuokoa wewe Mungu atatuokoa lakini wewe utaangamizwa na familia yako ‘ kuna mambo hayatakiwi kubadilika na sisi lazima injili isambae Tanzania nzima na kila mtaa usikiee majeshi majeshi mlokole asiye kata tamaa’ sasa esta akawaambia natakam niingie kwa mfalme kinyume cha sheria na wayahudi hawajui nini. Kila mtamgo ulio andaliwa na adui zangu nauangamiza kwa jina la Yesu mpango wa magonjwa mpango wa ajali mahali popote nauteketeza kwa jina la Yesu Amen.
Mfalme alivyo mwona Esta akamuuliza nini esta akamwambia uache maombi yako ya kuabudu mizimu uje nikuandalie chakula mfalme akatoka ndani akakaa na esta ” ukitaka kufungua moyo wa mtu mpe chakula kizuri awe Rp au Ms wewe mpe chakula” sasa akamwambia njoo nikuandalie chakula na mfalme akala akashiba na akamwambia naomba na kesho nikuandalie chakula lakini safari hii naomba na waziri wako haman nayeye aje kwenye chakula hiki watatu tu na biblia inasema haman alienda kuwaambia rafiki zake leo mimi ninakwenda kula kwa mfalme na mkewe maana yake Mungu akitaka kuwaangamiza adui zako anaanza kuwasogeza polepole na mwisho wao ni aibu wakati ule waraka wa kifu unatembea wayahudi walikuwa hawajui kuna mpango wa kuwakomboa unaendelea maana yake wakati wewe hujui shuda yako itaisha lini jua kuna mpango wa kukutoa kwenye tabu hiyo unaendelea.
 Basi Esta wakati akila chakula na haman na mfalme Esta akamwambia kuna mpando umeandaliwa wa mimi niuawe na tarehe imeandaliwa na mfalme akamuuliza ninani huyo ndipo akamwambia ni huyu haman na kwa hasira akaanza kutembea kwenye bustani na leo mfalme Yesu anatembea anaangalia. Na haman akaamua kumwangukia Esta miguun mwake na walewale walio panga mabaya juu yako wale watakusujudia kwa jina la Yesu maana yake shauri la  mtu mbaya huwa linageuka kuwa kitanzi kwa jina la Yesu. Yaleyale mlio nifanyia yawe kitanzi kwa jina la Yesu. Mfalme aliporudi esta akamwambia na Yule modekai ni mjomba wangu na nyumba ya nane haman amemuandalia msalaba wa kumsulubushia ndipo mfalme akaamuru akasulubiwe yeye mwenyewe na leo kwa jina la Yesu ule msalaba ulioandaliwa juu yangu uwasulubishe wao kwa jina la Yesu. Ndipo mfalme akaandika waraka mwingine wa kuwaruhusu wayahudi kuwa atakaye kuja kuwaua wamuue wao wenyewe na sisi tumeruhusiwa kuwasambaratisha waliojipanga kutuua kwa jina ya Yesu. Barua ikaandikwa na tareheh ilipofika wale maadui hawajui wakaenda na kuna waraka unasema vita sio vyenu vita ni vya Bwana na wao watataja magari na farasi sisi tuna mkono wa Bwana kwao kuna mkono wa wanadamu sisi tuna mkono wa Bwana wayahudi walipokwisha kujiandaa walijua kuwa wao sio kama wale na walisimama kupigana. Maisha yamejaa watu wabaya wenye nia ya kukurudisha chini na kukufanya uumie moyo usiogope. Sema nakataa aibu kwa jina la Yesu. Tumepokea waraka mimi ni rungu la Bwana na silaha zake za vita jeshi lijapo jipanga kupigana nami moyo wangu hauta ogopa Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu ni mwogope nani ikiwa Bwana yuko upande wetu ni nani aliye juu yetu kama vile mji wa Yerusalemu ulivyozungukwa na milima ndivyo Bwana alivyo wazunguka watu watakatifu wake. MIMI SIO KAMA WALE WALIOANGUSHWA NA KUONEWA KWA JINA YESU.

MAOMBI:
Katika jina la Yesu nawarudishia wao aliye andaa niharibu mimba namrudishia yeye aliye andaa mabaya imride yeye alieandaaa mikosi imrudie yeye mabaya yote yalioandaliwa nawarudishia wao na familia zao kwa jina la Yesu nawarudishia wao mauti iliyo andaliwa juu yangu nairudisha kwao kwa jina la Yesu mimi ni rungu la Bwana na silaha za Bwana katika vita nawafyeka kwa jina la yesu waliopanga vita name nawaponda kwa jina la Yesu  wachawi walioniloga kwenye kazi yangu nawafyeka kwa jina la Yesu nawateketeza kwa moto waroho Mtakatifu nawafyeka kwa jina Yesu walionitengezea mikosi na balaa nawa fyeka kwa jina la Yesu mimi sio kama wale.
Kwa jina la Yesu kuna mtu mahali aliyeandaa ubaya kwaajili yangu na familia yangu na familia yangu na kazi ninaamuru kuanzia sasa namfyeka aliyeandaa mabaya juu yangu aliye andaa mabaya juu ya kazi yangu namfyeka kwa jina la Yesu aliyeandaa juu ya ndoa yangu, kazi, masomo, ajali juu yangu na familia yangu namfyeka kwa jina la Yesu waliotega mitego naamuru kuanzia sasa mabaya yote yawapate wao kwa jina la Yesu. Imeandikwa Moto wa Bwana ni moto ulao naachilia moto uwale maadui wote kwa jina la Yesu
Wapo wanajua utakufa waambiee wewe hujafa kwa jina la Yesu tarehe ya leo ninaagiza kuanzia sasa kila aliyepanga mabaya kwaajili yako mabaya hayo yampate yeye na familia yake kwa jina la Yesu na kila aliyeandaa matatizo na aibu juu yako aibu hiyo haitakupata wewe itawapata wale walioiandaa kwa jina la Yesu na wanaotaka ufukuzwe kazi lakini wafuzwe wao kwa jina la Yesu. SEMA NIMESHINDAA AMEN. WEWE SIO KAMA WALE WALIOZOEA VYA KUNYONGA VYA KUCHINJA HAWAWEZI LAKINI WEWE UMESHINDA KWA DAMU YA MWANA KONDOO, MABAYA HAYATAKUPATA WEWE WALA TAUNI HAITAKUPATA WEWE.
 
 
Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe
 
 

Comments