Utangulizi
Zaburi 118: 1-29 (sitakufa bali nitaishi ili niyasimulie matendo ya Bwana)
I.
Somo
Maandiko ya msingi Luka 4:14- 24,
Daniel 5:2 -26
Bwana Yesu siku
moja alikwenda kwenye sinagogi mahali alipozaliwa na pale alipewa chuo cha nabii
Isaya ili asome na aliposema “ Roho wa bwana yu juu yangu kwa maana amenitia
mafuta, aliposema maneno haya yametimia
leo wayahudi walikasirika sana wakamtoa Yesu ili wamtupe kwenye ukingo wa mlima na kumwua. Wayahudi walikuwa
wamewatupa watu wengi kwenye ukingo lakini Yesu alipofika pale ukingoni alipita
kataikati yao kwa maana yeye siyo kama wale ambao walikuwa wakitupwa. Hii
inatufundisha kuwa hata wewe mtu uliyeokoka huwezi kupata madhara ya maadui
zako kwa maana mtu aliyeokoka ni tofauti na wengine, kwa hiyo uchawi, mitego na
majungu ya adui zako hayana nguvu juu
yako kwa jina la Yesu.
Leo
tunawatangazia adui zetu wote kwamba yale waliyowafanyia wengine hawawezi
kutufanyia kwa maana sisi siyo kama wale
kwa hiyo mambo yao hayawezi kutupata kwa
jina la Yesu. Sisi walokole wa kizazi cha
sasa siyo kama wale walokole wa kale walipopigwa shavu moja wakageuza na lingine,
waliponyang’anywa kanzu wakatoa na Joho sisi ni watu tofauti tumetumwa kutenda
na kutimiza kusudi la Mungu mpaka ulimwengu mzima wajue saa ya Ufufuo na Uzima,
kwa hiyo hakuna wa kutuzuia hata kama wamedondosha na kukatisha tamaa wengi
lakini sisi siyo kama wale , sisi tunazidi kusonga mbele kwa jina la Yesu.
Wayahudi
waliposikia Bwana Yesu anasema Roho wa Bwana yu juu yangu walifadhaika sana kwa
maana walijua maana ya Roho wa Bwana kuwa juu ya mtu. Roho wa bwana na anapokuwa
juu ya mtu , mtu Yule anakuwa na uwezo mkubwa wa kutenda lolote kama ilivyoandikwa
Roho wa Bwana akamjia Samson naye akawaua wafilist maelfu, Imeandikwa tena roho
wa bwana aliopokuwa juu ya Daud alimwua Goliath kwa hiyo aliposema hivyo
walisema huyu naye atapiga mtu . Vile vile aliposema Bwana amenitia mafuta
walitafakari kuwa watu wanaotakiwa kutiwa mafuta ni Nabii, Mfalme, Kuhani na
Vyombo vya Hekalu. Kwa hiyo waliogopa kwamba mafuta yale labda anataka kuwa
mfalme , au nabii kwa hiyo wakaona shaka na kuamua kumtupa ukingoni ili wamwuue
na kusudi la mafuta yale lisitimie lakini Yesu alipita katikati yao. Leo
nakutangazia mtu uliyeokoka mabaya waliokuandalia adui zako hayatatimia lakini
kusudi la Mungu litatimia kwako kwa jina la Yesu.
Vyombo vya
hekalu huwa havichezewi kwa maana vimetiwa mafuta, imeandikwa kwenye Daniel 5:2 -26 mfalmwe wa Babeli alipotumia
vyombo vya hekalu kwa ajili ya kunywea kwenye sherehe Mungu alikasirika na
kumwandikia maneno yafuatayo kwenye ukuta MENE MENE TEKELI NA PERESI, maana
yake ufalme wako umepimwa na kuonekana umepungua kwa hiyo amepewa mwenzako. Kwa hiyo mtu uliyeokoka ni chombo cha hekalu
na yeyote anayekuchezea anakatiliwa mbali na wengine wanachukua mahali pao kwa
jina la Yesu. Tunawatangazia hata viongozi wa Tanzania wanaowachezea watumishi
wa Mungu kuwa ufalme wao umepimwa na kuonekana umepungua kwa hiyo watapewa
wenzao.
Wayahudi
walifadhaika pia Yesu aliposema kuwa nimetiwa mafuta kuwatangazia wafungwa
kufunguliwa kwao. wayahudi walikasirika sana kwa maana ndani ya hekalu kulikuwa
na watu ambao wamewafunga watu kwenye magereza ya kiroho yaani kwemye magonjwa,
balaa, mikosi umasikini nakadhalika. Kwa sababu tabia za shetani ni kuwafunga watu bila kuwaachia kwenye magereza yake kama
ilivyoandikwa Isaya 14:17-18, Matendo 27:42 . kwa hiyo shetani na wakala wake walikasirika
sana waliposikia Yesu anataka kuwafungua watu kutoka kwenye magereza ya mateso.
Mungu naye mpango wake ni kuwaweka huru wafungwa kama ilivyoandikwa kwenye Yeremia
33 : 7, Zaburi 68:6, Ezekiel 16:53 Hosea 6:11,Nami kama mtumishi wa Mungu
leo nawatangazia wafungwa wote kufunguliwa kwao, wafungwa wa magonjwa, wafungwa
wa balaa, wafungwa wa madeni, wafungwa wa umasikini, wote nawatangazia uhuru
leo kwa jina la Yesu.
Wayahudi
walifadhaika pia Yesu aliposema kuwafanya vipovu wapate kuona tena, wayahudi
walikuwa wamewatia upofu watu wengi ili wafuate desturi za mafarisayo bila kuona
hatima yao.kwa hiyo Yesu alipotangaza
kuwafungua vipofu walikasirika sana kwa maana walijua udhalimu wao utadhihirika
mbele za watu . Nami mtumishi wa Mungu nawatangazia vipofu wa kiroho waone tena
, naondoa kila utando ulioweka kwenye macho ya watu ili wasione kwa jina la
Yesu. Nawatangazia Watanzania wote waliokuwa wametiwa upofu hata wasijue
kinachoendelea kwenye nchi yao naamuru waone tena na wajua hatima ya nchi yao
kwa jina la Yesu.
Wayahudi
walifadhaika pia Yesu aliposema nimekuja kuwaweka huru watu waliosetwa, maana
desturi ya mafarisayo ilikuwa kuwaseta (kuwagandamiza) watu na kuwaweka chini
ili wao wawe juu.
Nami mtumishi wa
Mungu nawatangazia kuinuliwa watu wote waliogandamizwa na magonjwa, umasikini,
madeni kwa jina la Yesu.
Wayahudi
walikasirika aliposema kuwa amekuja kuutangaza mwaka wa Bwana, kwa maana
wayahudi walikuwa na mwaka wa maachilio lakini walikuwa hawaachilie kama ilivyo
.kwa hiyo Yesu aliposema kutangaza maachilio ya wale wakosaji walikasirika
sana. Nami mtumishi wa Mungu nawatangazia msamaha watu wote waliofungwa kwa sababu ya shida zao
kwa jina la Yesu.
![]() |
maelfu wakiwa ndani ya bonde la kukata maneno |
II.
Ukiri
Kwa jina la Yesu , Roho wa Bwana yu juu
yangu kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri masikini habari njema,kuwatangazia
wafungwa kufunguliwa kwao na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa
na kuutangaza mwaka wa bwana uliokubaliwa.
III.
Maombi
Kwa damu ya Yesu
najitakasa, Bwana naomba upako wa kufanya vita dhidi ya wale waliotaka
nitumbukie kwenye mashimo ya uharibifu kwa jina la Yesu. Kwa damu ya Yesu
nawateka na kuwatumbukiza wao kwenye mashimo waliyoyaandaa kwa ajili yangu kwa jina la Yesu. Kwa jina la Yesu naamuru mtu yeyote aliyeandaa shimo la mauti,
magonjwa ajali na mikosi atumbikie
mwenyewe kwa jina la Yesu.
Imeandikwa kila achimbaye shimo atatumbukia
mwenyewe , naamuru mashimo yote waliochimba adui zangu watumbukie wenyewe kwa
jina la Yesu. Ninakataa kutumbikia kwenye shimo waliloliandaa kwa ajili yangu
au watoto wangu kwa jina la Yesu, nawatangazia adui zangu kuwa mimi siyo kama wale waliofanikiwa
kuwatumbukiza, nakataa kutumbukia kwenye shimo la magonjwa, balaa, mikosi umasikini na mauti, nakataa kuangamia nakataa
kuteketea kwa mitego na mashimo yao kwa jina la Yesu.
Imeandikwa kila
silaha itakayofanyika juu yangu haitofanikiwa, Katika jina la Yesu nawasukumia
nyie kwenye Mashimo ya mauti mliyoyachimba, naamuru silaha zote za maangamizi
mlizonitengeneza kwenye ulimwengu wa roho ziwanase wenyewe kwa jina la Yesu.
Imeandikwa sitakufa bali nitaishi nami niyasimulie matendo ya Mungu, nakataa kufa kwa ajali, magonjwa kuvamiwa au
kunyweshwa sumu kwa jina la Yesu. Naamuru mashimo yote ya mauti yaliyotengezwa
kwa ajili yangu yawameze adui zangu kwa jina la Yesu.
‘’AMEN’’
Comments