MKIKUBALI NA KUTII MTAKULA MEMA YA NCHI.


Na     Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.

BWANA YESU asifiwe.

karibu tujifunze habari njema zenye baraka.

Msilete Tena Matoleo Ya Ubatili; Uvumba Ni Chukizo Kwangu, Mwezi Mpya Na Sabato,kuita Makutano; Siyawezi Maovu Hayo Na Makutano Ya Ibada. Sikukuu Zenu Za Mwezi Mpya Na Karamu Zenu Zilizoamriwa, Nafsi Yangu Yazichukia; Mambo Hayo Yanilemea; Nimechoka Kuyachukua. Nanyi Mkunjuapo Mikono Yenu, Nitaficha Macho Yangu Nisiwaone; Naam, Muombapo Maombi Mengi, Sitasikia; Mikono Yenu Imejaa Damu. Jiosheni, Jitakaseni; Ondoeni Uovu Wa Matendo Yenu Usiwe Mbele Ya Macho Yangu; Acheni Kutenda Mabaya; Jifunzeni Kutenda Mema; Takeni Hukumu Na Haki; Wasaidieni Walioonewa; Mpatieni Yatima Haki Yake; Mteteeni Mjane. Haya Njoni, Tusemezane, Asema BWANA. Dhambi Zenu Zijapokuwa Nyekundu Sana, Zitakuwa Nyeupe Kama Theluji; Zijapokua Nyekundu Kama Bendera, Zitakuwa Kama Sufu. Na Kama Mkikubali Na Kutii Mtakula Mema Ya Nchi; Bali Mkikataa Na Kuasi Mtaangamiza Kwa Upanga; Maana Kinywa Cha BWANA Kimenena Haya.- Isaya 1:13-20.
BWANA YESU asifiwe.

Hapo juu tunaona vipengele vya mambo ambayo MUNGU wetu hataki tutenda.

1. MUNGU hataki matoleo ya ubatili.
Matoleo ya ubatili ni sadaka isiyo sahihi mfano huwezi kuipa pesa harafu ukasema ''ngoja niipeleke kanisani ili MUNGU anibariki zaidi''. hapo utakuwa unajidanganya wewe mwenyewe na huo ni ubatili mkubwa. matoleo ya ubatili ni pamoja na kupeleka sadaka isiyo sahihi mfano una laki 1 mfukoni lakini unamtoleaMUNGU Tsh. 100. hii sio haki na kumbuka kwamba hata hiyo laki moja uliyonayo ni MUNGU kakupa. na MUNGU hapa anaangalia tu utii wetu sio kwamba ana shida na pesa.

2.Uvumba ni chukizo.

3.Mambo yote unayoyatenda ukiunganisha na dhambi ndani yake ni machukizo kwa MUNGU.

4 Kuomba maombi mengi huku hujatubu dhambi zako haikusaidii, ni machukizo kwa MUNGU.

BWANA YEASU asifiwe.

Baada ya MUNGU kuonya na kututaka tuache uovu wote hatimaye anasema baada ya kutubu kwetu toba ya kweli atatusamehe na hakika atataka tusemezane naye lolote tunalohitaji katika mapenzi yake atatupa.

Sehemu pekee ya kueleza mambo yako ni kwa MUNGU,

Unikumbushe – MUNGU anaposema tumkumbushe hana maana kuwa amesahau. Hapana. Ila anataka kuona moyoni umeweka nini. aliwaambia wana wa Israel kuwa “Niliwazungusha makusudi ili nione mioyoni mwenu mna nini.” Ndiyo maana tunatakiwa kuliweka Neno la BWANA mioyoni mwetu. Zab 119:10.

MUNGU anatupenda sana na hakika tukikubali na kutii tutakula mema ya nchi.
ona hapa jinsi upendo wa MUNGU kwetu ulipo.

2 Korintho 6:18 ''Nitakuwa BABA kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike.''

Andiko hili linatufundisha kwamba MUNGU anatupenda wanadamu wote bila kujali jinsia zetu.
Biblia hapo inaonyesha kwamba kama mwanamke au mwanaume atampa BWANA YESU maisha yake, atakuwa ametengwa mbali na shetani na ataingia katika kundi la watoto wa MUNGU wenye haki sawa mbele zake bila kujali jinsia zao.
 

 Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisha kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292

                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

 MUNGU Akubariki.

Comments