MUNGU AJIDHIHIRISHA KATIKA IBADA KPC KAWE.

Pasto Yona Gida akiombea
Kutoka KPC jana kulikuwa na ibada yenye nguvu za MUNGU.
Katika ibada hiyo mhubiri alikuwa ni Mchungaji Yona Gida kutoka Arusha ambaye alihubiri na kuombea, hakika ilikuwa ni siku ya maajabu ya kupokea  baraka za MUNGU na kufunguliwa kutoka vifungo vyote.

Mchungaji Yona Alifundisha somo liitwalo SIRI KUBWA ILIYO KATIKA UTOAJI KANISANI.
Ni ujumbe wa maajabu hakika maana mambo yaliyofundishwa jana ni muhimu sana kwa kila mwanadamu.

Mhubiri alisema Kuna siri kubwa sana katika utoaji. MUNGU anahitaji unyenyekevu  na moyo uliopondeka wa utoaji.
 Mahali itakapokuwapo hazina yako yaani sadaka yako ndipo kutakuwapo pia na Roho yako.
Jambo jingine alizungumzia kuhusu MUNGU anahitaji nini katika sadaka au zaka yako?
Je huwa unakumbuka kupeleka zaka kamili kanisani au unapeleka robo?
Huu ni ujumbe wa siri kuu ya kubalikiwa.
Zifuatazo ni picha katika ibada ya jana kutoka Kawe Pentecostal Church.









Wakati wa kumsifu MUNGU.

MCHUNGAJI YONA KATIKA MAOMBI KABLA YA NENO.

Kumsifu MUNGU kunawapasa wanyoofu wa wote. hapa ni wakati wa kumsifu MUNGU katika Roho na kweli.

Ni furaha nyumbani mwa BWANA

Mwimbaji binafsi Teddy Lukindo akiimba wakati wa ibada.

Elshadai group wakiimba.

KPC choir wakiimba wakati wa ibada.

Ni wakati wa maombezi na kufunguliwa. Hapa Mchungaji Yona Gida akiombea wenye mahitaji mbalimbali.



ni wakati wa kupokea baraka za MUNGU.

Wanafunzi mbalimbali wakiombewa.


Comments