MUNGU ALINIPONYA NA AJALI MLIMA KITONGA.

Ndugu Ibrahim Ezekiel akishudia matendo makuu ya Mungu aliyomtendea
Ndugu Ibrahim Ezekiel alishuhudia katika kanisa la E C W C Worship center jijini Dar es salaam  jinsi Mungu alivyomponya kwa ajali iliyokuwa ikimkabili wakati akiendesha gari (Lori) mlima wa Kitonga kuelekea Daresalaam.

Akibakiza kona Sita kuumaliza mlima ule Lori hilo aina ya scania likiwa na mzigo wa tani 35 lilifeli breki na hivyo kupoteza udhibiti wake,alimwamuru utingo wake aruke nje ili kujinusuru na ajali iliyokuwa ukiwakabili na ndipo alimwita Mungu na Hakika Likiwa katika mwendo wa spidi 120 km kwa saa liliweza kukata kona zote Kali na kufuata uelekeo wa barabara mpaka liliposimama lenyewe.

HAPA ILIKUWA NI KIPINDI CHA SHUHUDA, WATU WAKISHUHUDIA MAMBO MAKUU AMBAYO BABA WA MBINGUNI AMEWATENDEA.

Hakika Ni mkono wa Mungu tu ulioyatenda haya.sifa na utukufu tunamrudishia yeye.



Comments