![]() |
Kifungo cha miezi mitatu jela alichohukumiwa mwimbaji wa muziki wa
injili nchini Happy Kamili na mahakama ya mwanzo mkoani Mbeya, hatimaye
kimebadilishwa na sasa kitakuwa kifungo cha nje cha miezi mitatu huku
akitakiwa kuripoti kwa mkuu wa jela kila siku asubuhi. Happy Kamili
alihukumiwa kifungo hicho na mahakama ya mwanzo mkoani Mbeya kutokana na
kuendesha gari kizembe wakati anarudi nyuma na kugonga gari nyingine.
Taarifa za kubadilishwa kwa hukumu hiyo ya awali ambayo ilipokelewa kwa
masikitiko na wadau wa muziki wa injili wanaotumia mitandao ya kijamii,
imepatikana kupitia kwenye ukurasa wa Facebook ya mmiliki wa blogu ya
Mbeya yetu bwana Joseph Mwaisango. Happy Kamili ambaye ni mke wa
mchungaji Athanase Kamili wa kanisa la E.A.G.T Isanga Mbeya, amejulikana
zaidi kwenye muziki wa injili nchini kupitia nyimbo zake kama 'Huwezi
kubeba mzigo mwenyewe, Mpango wa Mungu lazima utimie…. alilopanga Mungu
ninani apingee…
Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu blogu ameripoti hivi kupitia ukurasa wake wa Facebook
Breaking Newsss mwimbaji wa nyimbo za injiri Happy Kamili aachiwa
ila ataendelea kutumikia kifungo chake cha miezi mitatu akiwa nje ya
gereza na kuripoti kila siku asubuhi kwa bwana jela
ASANTE BWANA YESU KWA MUUJIZA HUU.
Kama hukusoma hukumu ya kwanza FUNGUA HAPA
Angalia video ya wimbo wa Happy Kamili iitwayo DHABIHU ZA SIFA.
Comments