MWALIMU WETU NI MMOJA TU BIBLIA(NENO LA MUNGU)




Paulo Mtume akasema;
"Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo TULIOWAHUBIRI NA ALAANIWE...."
Gal 1:8-9.

Wapendwa wangu, ikiwa sisi ni wanafunzi wa Yesu, Imetulazimu kuyachunguza maandiko!
Tunaona nyakati za Paulo na Sila watu wa Beroya waliyachunguza maandiko
Mdo 17:10-11
Na hiyo ni haki ya kila mwanafunzi wa Yesu, Maana biblia imetutahadharisha mapema, tusiziamini kila Roho bali tuzipime hizo Roho kama zimetokana na Mungu au la
1Yoh 4:1

Na katika kuyachunguza maandiko hapo ndipo tutakapogungua kuwa TUMEZUNGUKWA NA WALIMU WENGI WA UONGO.
Yak 3:1

Hivyo basi; niwasihi wapendwa wangu katika Kristo Yesu! Tusibabaishwe na majina makubwa makubwa waliojipachika baadhi ya Watumishi wa Mungu: Mfano NABII, MTUME, MCHUNGAJI, ASKOFU,MWALIMU, MWINJILISTI NK
‪#‎Tutawafuata‬ wao, na Majina yao, ikiwa wao nao wanafuata KWELI YA NENO LA MUNGU na siyo vinginevyo.

‪#‎Ukiona‬ kiongozi wako anakuambia usifuate matendo yangu bali fuata neno la Mungu,
Tambua fika huyo ni kiongozi kipofu, hafai kukuongoza!

‪#‎Yesu‬ alikuwa kielelezo chetu, alitenda kwanza ili nasi tumfuate
Mdo 1:1

‪#‎Paulo‬ Mtume akasema; mnifuate mimi kama mimi nilivyomfuata Kristo
1kor 11:1

Sasa huyo anayekwambia usimfuate yeye ametoa wapi hayo mafundisho? Maana kiongozi yoyote yule, anapaswa kuwa Kielelezo kwa wengine!

UKIYAONA HAYO:
Ni thahiri shairi kuwa huyo ni wa baba wa uongo  yaani Ibilisi,Hafai kukufundisha, atakuambukiza Roho za Ibilisi tuu, taka usitake!


USHAURI WNG KWAKO:

Kimbia ndugu yangu uiponye Roho yako!


Mungu akubariki, kwa kuusoma ujumbe huu! 
Ni maombi yangu kwa Bwana kuwa utaanza kuwachunguza hawa viongozi wetu kwa kutumia Neno la Mungu (BIBLIA) Kisha utachukua hatua!

Mungu akupe macho ya Rohoni upate kuyaona haya dhahiri! Na akupe mwongozo wa nini ufanye! Ameen
 
Ubarikiwe na Bwana,
Shaloom Shaloom!

By Lucy Marandu.

Comments