| Hilo ni pigo jipya kwa Kanisa Katoliki ambalo kwa siku za karibuni lina kilio cha kutaka mapadri waruhusiwe kuoa huku Papa Francis akieleza msimamo wake kuwa angependa kuendelea kuwa na mapadri waseja | 
Uamuzi huo ambao unauweka mtandao huo katika 
hatari ya kutengwa na Makao Makuu ya Kanisa Katoliki duniani (Vatican), 
umefanyika mwishoni mwa wiki baada ya mwanamke huyo kutangazwa kasisi wa
 kwanza nchini Marekani.
                
              
Alikuwa miongoni mwa wanawake wa kwanza kuhudhuria masomo ya tauhidi (theolojia) katika Chuo Kikuu cha Marquette miaka ya 1960.
                
              
Lewis alisema kashfa za karibuni kwenye kanisa 
hilo na kutengwa kwa baadhi ya watu ni moja ya mambo ambayo yamemchochea
 kufikiria kupanda kwenye mimbari na kuhubiri.
                
              
“Nimedhamiria kuonyesha njia kwa wengine kwamba 
wanawake tunayo nafasi kubwa ya kuongoza kanisa kama makasisi. Nina 
mabinti wanne. Hakuna hata mmoja ambaye anasali kwenye kanisa hilo 
(Katoliki),” Lewis aliliambia shirika la ABC News. 
“Wamekerwa na matukio ya siku za nyuma, kashfa ambazo zimeliandama kanisa … wanasema Ukatoliki umebakia kuwa wa kwangu, si wao.”
                
              “Wamekerwa na matukio ya siku za nyuma, kashfa ambazo zimeliandama kanisa … wanasema Ukatoliki umebakia kuwa wa kwangu, si wao.”
Sherehe za upadrisho wa Lewis zilizofanyika 
Jumamosi, zilihudhuriwa na wageni 200 kwenye eneo la nyumba yake. 
Miongoni mwao walikuwa ni viongozi wa dini isipokuwa wale wa Kanisa 
Katoliki. Lewis ni mwanachama wa mtandao wa Roman Catholic Womenpriests 
ambao ulianzishwa mwaka 2002 na umekuwa ukitaka ushirikishi, kumjua 
Kristo zaidi kwenye karne ya 21 … wenye mtazamo wa kumfuata Yesu 
kikamilifu kwa kuwahusisha wanawake kama mitume na watu sawa kama ilivyo
 katika Injili.
  
                
              
Maofisa wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Michigan 
ambao hawakuhudhuria sherehe hizo walieleza kuwa waumini wake 
walioshiriki sherehe hizo batili nao watashughulikiwa.
                
              
Askofu Paul Bradley wa Jimbo Katoliki Kalamazoo, 
alitoa tamko kali kupitia mtandao wa WWMT-TV in Kalamazoo, Mich., 
akieleza kuwa yeyote aliyeshiriki shughuli hiyo hatambuliwi na Kanisa 
Katoliki.
                
              
Mbali ya kuonywa na jimbo hilo, Lewis alisema 
shughuli hiyo ilikuwa yenye mafanikio na alitarajia kuwa ingepingwa na 
Kanisa Katoliki. Hata hivyo, alisema licha ya kupewa daraja hilo, 
hafahamu jukumu ambalo atapewa na kanisa.
                
              
Alisema majirani zake na mwanawe wa kiume na 
mchumba wake, walimuunga mkono baada ya kutambua nafasi ya mwanamke kama
 kasisi na kusema yuko tayari kuwafungisha ndoa wapenzi hao.
                
              
Hilo ni pigo jipya kwa Kanisa Katoliki ambalo kwa 
siku za karibuni lina kilio cha kutaka mapadri waruhusiwe kuoa huku Papa
 Francis akieleza msimamo wake kuwa angependa kuendelea kuwa na mapadri 
waseja.
Comments