MWENDO WA CHOMBO CHAKO UKOJE?



 
BWANA YESU asifiwe.


MUNGU ameutunza  ujumbe huu ndani yangu kwa muda mrefu sana, leo naomba tujifunze pamoja.


MWENDO WA CHOMBO CHAKO UKOJE?

Mwendo ni IMANI.

Chombo ni WOKOVU.

Kwahiyo ujumbe huu tunaweza tukauita kwamba ‘’IMANI YA WOKOVU WAKO IKOJE?


Kumbuka kwamba tunapozungumzia Chombo na Mwendo ina maana kuna safari na tayari chombo kipo njiani kikielekea sehemu Fulani.


Kwa habari ya wateule wa MUNGU safari yetu haina kituo  na kituo chetu ni kimoja tu yaani  yaani mbinguni  ukitaka kushuka unashuka wewe lakini watakatifu safari badi inaendelea.

Waebrania 11:1,6  ''Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana,  Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye MUNGU lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao''

Hapo kwenye hilo andiko tunaona mwendo ambao mwanadamu anatakiwa atembee nao.

Imani ni mwendo, imani ni ya muhimu sana. Wengi wana imani lakini imani zao sio za kumwabudu MUNGU aliye hai anayepatikana katika KRISTO YESU pekee.

Imani ya kweli ya uzima ni imani katika MUNGU aliye hai na Biblia katika Wakolosai 2:2 b inasema ''KRISTO ni siri ya MUNGU '' maana yake ukitaka kumwabudu au kumfahamu MUNGU wa kweli basi MUNGU huyo anapatikana katika KRISTO YESU. 


Je wewe ambaye uko kwenye Chombo(wokovu) mwendo (Imani) wako ukoje? Je unasua sua au mawimbi yanataka kukuzamisha baharini(duniani?) 


Katika chombo chako ni changamoto gani unazokutana nazo?

Ufanye nini ili uende salama kwenye chombo chako?



Ndugu yangu mteule wa MUNGU nakuomba katika katika changamoto zako usisitesite wala kurudi nyuma.

Mtegemee YESU huyo huyo  uliyemtumaini tangu mwanzo.

Unapokutana  na changamoto  katika safari yako ni kipi kinachokupa nguvu? Ni kipi unategemea Biblia ina jibu juu ya nani wa kumtegemea wakati wa changamoto ndani ya chombo chako Luka 4: 1-12 (''a YESU, hali amejaa ROHO MTAKATIFU, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na ROHO muda wa siku arobaini nyikani, akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa.  Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa MUNGU, liambie jiwe hili liwe mkate.  YESU akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu. Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.  YESU akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie BWANA MUNGU wako, umwabudu yeye peke yake. Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa MUNGU, jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde; na ya kwamba,mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. YESU akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu BWANA MUNGU wako.''

=YESU alimtegemea ROHO MTAKATIFU  ambaye ndiye aliyemuongoza.

BWANA YESU asifiwe.

=Huyo unayemtegemea anapata faida gani au  hasara. 
Isaya 61:1-3 ''Roho ya BWANA MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha MUNGU wetu; kuwafariji wote waliao;  kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.''

=Hasara kama tukitumia akili zetu wenyewe

 Mithali 23:4
 ''Usijitaabishe ili kupata utajiri; Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe.'' 

 =Hakika ni hasara kubwa kama tukizitegemea akili zetu wenyewe.

Je mwendo wako ni wa kusitasita au ni wa kumaanisha pale unapopita kwenye mabonde au milima?  

Ayubu 5:1-2 ''Haya, ita sasa; je! Yuko atakayekujibu? Nawe utamwelekea yupi katika hao watakatifu?  Kwani hasira humwua mtu mpumbavu, Nao wivu humwua mjinga.''

=Ukiwa hapa duniani  mwangalie tu aliyekuita tu .

Hata dhahabu lazima ipite kwenye moto ndipo iwe dhahabu safi

 Yoshua 1:7 ''Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako''

=Ndugu zangu lazima tutambue kwamba kwenye safari yetu lazima tutakutana na nyakati tofauti tofauti lakini nakuomba linda moyo wako kuliko yote uyalindayo harafu linda macho yako  na pia linda kinywa chako. 

 2 Timotheo 3:1 ''Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. ), Mhubiri 3:1 ( Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. ), 2 Timotheo  3: 12-13 (Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika KRISTO YESU wataudhiwa. lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. ''

=Tukumbuke kwamba safari yetu haina kituo  na kituo chetu ni kimoja tu yaani mbinguni. Ukitaka kushuka  unashuka wewe tu lakini safari kwa watakatifu inaendelea kama kawaida .
 Mathayo 25:1-10.

=Tuongeze mafuta ya taa zetu  ambayo ni kujitakasa na kuongeza maombi 
Isaya 61:10 '' Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika MUNGU wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu'' 

 =Tufurahie wokovu wetu.

Katika mwendo wa chombo chetu kuna ushindi mkubwa.

 Ayubu 19:25 ''Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi''

=Kuna ushindi mkuu kwa wateule maana BWANA YESU alikwisha tushindia pale msalabani ndio maana hata majina yetu yakaandikwa kwenye kitabu cha uzima mbinguni maana tumeokoka na tunaishi maisha ya wokovu.
 

Wafilipi 4:4-7,13 ''Na amani ya MUNGU, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika KRISTO YESU. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.''
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           +255714252292
                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
 MUNGU Akubariki.


Comments