![]() |
Jana nimestushwa sana kwa taarifa ya kuhukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela rafiki yetu ,mtumishi wa MUNGU na mwimbaji wa nyimbo za injli Happy Kamlili kwa kosa la kuendesha gari kiuzembe na kugonga gari nyingine(alipokuwa akirudi nyuma) january 2014.
Najua ni wakati mgumu sana kwa Mchungaji Athanase Camillly ambaye ni mme wa Happy Kamili ,watoto na washirika wa EAGT Isanga Mbeya.
Tumwombee mtumishi wa MUNGU huyu kwa yote.

Mwanamuziki huyu anayetamba sana na wimbo wake "Mpango Wa Mungu" na "Jina Kubwa" amehukumiwa kifungo cha Miezi Mitatu Jela bila faini katika Mahakama Ya Mwanzo Mkoani humo kwa Kosa la Kusababisha ajali ya barabarani.
Kesi hiyo iliyokuwa imeanza kusikilizwa mwezi January Mwaka huu, siku ya jana imetolewa hukumu kwa Mwanamuziki huyo Kupatikana na hatia ya kusababisha ajali kwa kugonga gari lingine kwa nyuma. Mwanamuziki huyo baada ya Kukiri kutenda kosa hilo mahakamani alipatikana na hatia ya Hakimu alitoa Hukumu ya Miezi Mitatu Jela pasipo kutoa Hukumu Mbadala ya Faini.
![]() |
Mchungaji Kamili ambaye ni mme wa Happy Kamili. |
Happy Kamili ni mmoja wa waimbaji bora kabisa kwangu .
ona hapa nyimbo zake mbili ambazo mimi binafsi nazipenda sana.wimbo wa mpango wa MUNGU na HUWEZI KUBEBA MZIGO HUO MWENYEWE.
Comments