NGUVU YA KUPITA

Kutana na Mtu wa Mungu,Nabii Samson pale katika Hema ya Kinabi Nyankumbu Mkoani Geita Tanzania,


Utangulizi:                                

kuna watu wengi sana wamezuwiwa maeneo Mali mbali  katika ulimwengu wa Kiroho  wamezuhiliwa kuona walichotakiwa kuona, kusikia walichotakiwa kusikia, kusema  walichotakiwa kusema,kiafya  magonjwa hayawaachi wakapumuwa, nyuma zimegeuka Maduka ya Dawa,kielimu wanapenda kusoma lakini hawaelewi kabisa, Ondowa kizuwizi upite,unahitaji Nguvu ya kupita,

Nguvu ya Mafanikio ya kila jambo linalofanyika  katika hii Dunia ni matokeo mazuri ya Maandalizi  Mazuri yaliyoambatana na uhuru wa kutenda lile unalolitaka lifanyike, na kila jambo unalotaka kulifanya linaupizani, na ili ufanikiwe unahitaji Nguvu ya kupita ile ya upinzani, Mafanikio ya watu yamezuhiliwa  katika ulimwengu wa kiroho,

Kupita nini,

Kupita ni kutimiza Lengo lako ulilokusudia kulifaya,

Malengo ya watu wengi yamezuwiliwa  na watu wengine wanajuwa na wengine hawajui, kama umezuiliwa Huwezi kufanya chochote Mtu akipelekwa sero wanasema yuko kizuwizini, ulikuwa unafanya biashara,uchumba Masomo biashara Huwezi tena,

Hesabu 20:21 Basi hivyo Edomu akakataa kumpa Israeli ruhusa kupita katika mipaka yake; kwa hivyo Israeli akageuka na kumwacha.

Tunajifunza hapa Wana wa Israel wamezuiliwa kupita wakageuka, kushindwa kupita maana yake  Nguvu uliyonayo au mamlaka uliyonayo ni Ndogo kuliko ile Nguvu iliyokuzuwia

Madhara ya kuzuhiliwa kupita,

v  Unaweza kujikuta unageuza Malengo yako

v  Unaweza ukatofautiana na hatima ya maisha yako,

v  Unaweza ukachelewa kufika katika hatima yako

v  Unaweza kujikuta unakata tamaa ya kuendelea mbele,

v  Unaweza ukatumikishwa japo hutaki,

Kizuwizi katika maisha ni kitu kibaya sana,  unahitaji Nguvu ya kukuwezesha kupita,

Isaya 43:16 Bwana asema hivi, yeye afanyaye njia katika bahari; na mahali pa kupita katika maji yenye nguvu;

Kukubali Mungu akatawala maisha yako ni kukubali kupia maana yeye  kwanza ni njia ya Uzima na anafanya njia  katika bahari  mahali pa maji yenye Nguvu Hivyo hunasababu ya kugeuza njia,au kufanya maarifa yako  yatakushinda kubali mwenye njia akupe njia ya kupita,

Kila mtu anayezaliwa Mungu anakuwa amemwandalia njia yake katika mpangilio mzima wa maisha yake kinacho leta shida watu wanaziharibu hizonjia wao wenyewe kwa kutofuata maelekezo yale ya Mungu aliyoweka,

Mwanzo 6:12 Mungu akaiona Dunia, na tazama, imeharibika; maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani.


Kwanini njia inaharibika,

Ayubu 19 : 8 Yeye ameiziba njia yangu nisipate kupita, Na kutia giza katika mapito yangu.
9 Amenivua utukufu wangu, Na kuiondoa taji kichwani mwangu Njia inaharibika kwakupoteza mahusiano na Mungu Ibilisi alichokitaka kwa Ayubu ni kumfarakanisha yeye na Mungu akatumia Mbinu Mbali mbali  kuharibu njia  ili ayubu akose msaada wa ania yeyote,

Kunasomo nzuri la kujifunza hapa kwa Rafiki yetu Ayubu,

Nataka umfahamu adui na Baadhi ya Mbinu anazozitumia kukuharibia Mahusiano yako na Mungu njia ikiharibia fahamu hakuna safari,

Sisi tu wasafiri hapo ulipo fahamu hivyo Hapa Duniani ni kakituo tu  sasa Tunapoendelea na safari yetu ukipoteza njia umepotaza safari, umepoteza Hatima,Muovu anajaribu kujifunuwa  kwa matukio mbali mbali ili usimfahamu kuwa ni yeye, lakini ndivyo alivyo, kibinadamu haya matukio yaliyompata Ayubu  Angeweza kujikuta ameharibu njia na akapoteza Mahusiano,

Hebu tumwangalie Muovu jinsi anavyoweza kujificha ndani ya vitu, akashambulia kwa matukio yaliyopambwa majina,tofauti tofauti,

Ayubu 1:10

v  Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao

v  Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza


v  Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga

Nikatafakari nikisema, Nimejipatia hekima nyingi kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; naam, moyo wangu umeona kwa wingi hekima na maarifa.

v  Upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa;

Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia;
21 akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe.
22 Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu


Isaya 43:17  atoaye gari na farasi, jeshi la askari na uwezo; wamelala, hawataondoka; wametoweka, wamezimwa mfano wa utambi.


Sitaki kujuwa wewe au aliyekuziwia ni nani ninachokifahamu ni kitu kimoja Yupo mwenye uwezo wote, anayefanya njia baharini katika maji yenye Nguvu,

Anayeondoa Magari na farasi Jeshi la Askari na uwezo,

Wote watakao niona watalala Hawataondoka, watazimwa kamo utambi,

Omba Maombi Haya simamia maandiko ya kuondoa Maadui katika njia yako  yaani anza na Toba Nipo URuhusu Nguvu za Bwana zi kawatawanye Maadui  kisha wa lale, walaze usingizi wewe upite,

Yeremia 10:23 Ee Bwana, najua ya kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu.


Danieli  8:24  Na nguvu zake zitakuwa nyingi mno, lakini si kwa uwezo wake mwenyewe; naye ataharibu kiasi cha kustaajabisha watu, na kufanikiwa, na kutenda apendavyo; naye atawaangamiza hao walio hodari na watu watakatifu.


Mtu asiye haki ni fidia ya wenye haki; Naye afanyaye hila ni badala ya watu wa adili.

Mithali 21:18

Pata Mosomo mengine mengi ya Mtu wa Mungu Nabii Samson

Upenyo wa kumiliki

siri kuu tatu za kutunza siri zako zote

Nguvu ya kinya 

Ushindi katikati ya vita

jifunze kusamehe,

Hatima iliyopindishwa

yapo mengi unaweza ukaagiza ukapata

 0756 809 209 Mtu wa Mungu anaptika wakati wote yupo hewani

Comments