Hili ni swali ambalo mara nyingi huuulizwa na wale ambao siyo Wakristo, wakituuliza sisi Wakristo, ni sababu ipi iliyopelekea sisi tuoe wakati Yesu yeye hakuoa? na ukizingatia kuwa Yesu alisema tujitie nira yake na tujifunze kwake, kwa kuwa yeye ni mpole na mnyenyekevu wa Moyo, (Mathayo 11:29), hili ni swali zuri ambalo sisi Wakristo tunapaswa kulijibu swali hilo, kwa kuwa ndivyo ambavyo tumehimizwa kutoa majibu kwa maswali ambayo tunaulizwa. 1 Petro 3:15 Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.
![]() |
Na Abel Suleiman Shiriwa. |
KUWA NI KWA NINI YEYE HAKUOA NA SISI TUNAOA?.
Luka 20:34 Yesu akawaambia, Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa. Yesu anasema kuwa, wale ambao wanastahili kuoa na kuolewa ni wale wana wa Ulimwengu, kwa kuwa sisi Wakristo tupo katika Ulimwengu huu ndiyo maana watu wanatushuhudia WANAUME tukioa, na WANAWAKE wakiolewa, sasa KWA KUWA wanaooa na kuolewa ni wana wa Ulimwengu huu, Je! Yesu nae ni miongoni mwa wana wa ulimwengu huu ili awe na sifa za kuoa? ngoja tuuulize yeye mwenyewe. Yohana 8:23 Akawaambia, Ninyi ni wa chini, mimi ni wa juu; ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu.
YESU YEYE SI WACHINI BALI N I WA JUU NA YEYE SIYO WA ULIMWENGU, NA NDIYO MAANA HAKUOA WALA KUOLEWA, KAMA AMBAVYO SISI WAKRISTO TUTAKAPOKUWA KWENYE ULIMWENGU AMBAO YUPO YESU, yaani Ulimwengu mpya, Wanaume hatutaoa wala wala wanawake hawataolewa, kwa kuwa tutakuwa tumekwisha kutoka katika Ulimwengu huu wa kuoa na kuolewa. Luka 20:35 lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi; 36 wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo.
MUNGU akubariki sana .
By Abel Suleiman Shiriwa.
Comments
pia kuna sehemu akaoma akasema
hawa sio wa ulimwengu huu kama mm nisivyo wa ulimwengu huu ila siombi uwatoe ulimwenguni bal uwalinde na yule mwovu. ulichofafanua sio logical mkuu tengeneza hoja