NI MWEZI WA 6 SASA HEBU TUPATE TAFSIRI YA NAMBA 6 KATIKA MAANDIKO.

Na Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministries (VHM).
.

1. Namba SITA ni namba ya Mwanadamu na inaonyesha jinsi ambavyo Mwanadamu asivyo kuwa mkamilifu.

2. Mwanadamualiumbwa katika siku ya SITA.

3. Mungu alisema Siku SITA ni siku za Mwanadamu kufanya kazi.

4. Kuna vizazi SITA vilivyorekodiwa kwa Kaini ambapo maandiko yanasema kilikuwa ni kiovu sana.

5. Goliath alikuwa na silaha za aina SITA.

6. Katika Mwanzo 22, tunapata sadaka za kuteketeza imetajwa mara SITA ikionyeshwa kama sadaka ya Mwanadamu.

7. Kwa wayunani mtumwa alitakiwa kutumikia miaka sita na kutolewa katika mwaka wa 7. Miaka sita walikuwa maalumu kwa ajili ya ardhi kwa kupandwa na kuvunwa.

8. Katika majaribu ya Yesu na Kusulubiwa, kuna watu SITA walio shuhudia kuwa Yesu hakuwa na kosa la kumfanya asulubiwe. (Pilato Luka 23:14, Herode Lk. 23:15, Judas Mt. 27:19, Mwizi msalabani Lk. 23:41).

Comments