REUVIN RIVLIN: RAIS MPYA WA ISRAELI.

Reuven Rivlin amechaguliwa na bunge la Israel 10.06.2014 kuwa rais mpya wa taifa hilo la kiyahudi akichukuwa mahala panapoachwa na Shimon Peres
Rais mteule wa Israel Reuven Rivlin
Rais mteule wa Israel Reuven Rivlin
Rivlin ambaye ni mwanachama wa chama tawala cha mrengo wa kulia cha Likud anakuwa ni rais wa 10 wa taifa hilo anayetwaa nafasi ya Shimon Peres anayeachia madaraka mwezi Julai.
Akitangaza ushindi huo wa Reuven Rivlin,spika wa bunge la Israel Yuli Edelstein amesema Rivlin amewashinda katika kinyang'anyiro hicho mpinzani wake wa mrengo wa kati Meir Sheetrit kwa kura 63 dhidi ya 53 katika zoezi la upigaji kura kwa siri katika bunge la nchi hiyo lenye viti 120.
Rais Schimon Peres na mwenzake wa Palestina Mahmoud Abbass
Rais Schimon Peres na mwenzake wa Palestina Mahmoud Abbass
Rivlin amewahi kuwa spika wa bunge mara mbili na ni mtu anayetajwa kuwa mwenye msimamo thabiti katika kupinga azma ya kuundwa kwa dola la wapalestina na vile vile amekuwa daima akiunga mkono ujenzi wa makaazi zaidi ya walowezi katika ardhi ya wapalestina iliyonyakuliwa kwa mabavu na Israel.Ni mwanasheria na mtu ambaye anafahamika sana katika juhudi zake za kutetea demokrasia na haki za kiraia ambazo zimempa heshima kubwa katika upande wa mrengo wa kushoto na hata miongoni jamii ya waarabu waliowachache katika taifa hilo la kiyahudi.
Hata hivyo rais huyo mteule wa Israel mwenye umri wa miaka 74 atakuwa na kibarua kigumu kufuata nyayo za rais anayeondoka madarakani Shimon Peres ambaye haiba yake na umaarufu ulimpa nafasi ya kutumia wadhifa wake wa urais ambao hauna mamlaka makubwa katika kuueneza au kuupa nguvu ujumbe wa amani katika ngazi ya kisiasa.Wengi wa wadadisi wa mambo wanaashiria kwamba baada ya kuondoka Peres madarakani mwezi Julai huenda mwelekeo wa siasa za Israel ukajikita kutoka kwenye mrengo wa Kimataifa na kuzingatia zaidi masuala ya ndani.
Katika Duru ya mwanzo wabunge walipiga kura kuamua juu ya wagombea watano waliojitokeza kugombea nafasi hiyo akiwemo Dalia Itzik mwanamke wa kwanza kuwahi kushikilia nafasi ya spika wa bunge la Israel,Knesset,jaji msatafu wa mahakama kuu Dali Dorner na mshindi wa tuzo ya Nobel ya Kemia Dan Shechtman.
Waziri mkuu Benjamin Netanyahu akiwa bungeni
Waziri mkuu Benjamin Netanyahu akiwa bungeni
Hata hivyo Ushindi wa Rivlin umekuja katika duru ya pili ambayo ni ya mwisho ya mpambano huo dhidi ya mgombea wa chama cha mrengo wa wastani cha Hatenua,Meir Shitrit.Pamoja na kuwa anapinga fikra ya kuwepo dola la wapalestina katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza anawafiki ushirikiano zaidi na waarabu na hata hatua ya kuwapa uraia wa Israel wapalestina zaidi.
Shimon Peres rais anayestaafu
Waziri mkuu Benjamin Netanyahu ameupongeza ushindi wa Rivlin akisema anataraji ushirikiaono wa karibu na rais huyo mteule ambaye mamlaka yake sio makubwa lakini anauwezo kiasi katika masuala muhimu,ikiwemo katika utoaji wa msahama kwa wafungwa pamoja na kumteua waziri mkuu mpya baada ya uchaguzi.Rais anayeondoka Shimon Peres ana umri wa miaka 90 na amekuwa rais wa Israel tangu mwaka 2007 baada ya kuondoka Moshe Katsav aliyeshtakiwa kwa tuhuma za ubakaji.Hata hivyo dalili zote zinaonyesha kwamba Peres ambaye ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel ataendelea kujihusisha na siasa ingawa inaonekana hatokuwa na wadhifa wowote wa kisiasa katika taifa hilo kwa mara yake ya kwanza katika kipindi cha miongo mingi.

Comments