RIPOTI: NIGERIA KINARA KWA MATESO YA WAKRISTO


Kifungo ©Stand up for the truth
Taarifa mpya ya utafiti imeanika wazi kwamba taifa la Nigeria ndio nchi ambayo wakristo nchini humo wanaishi kwa mateso makubwa, ikilinganishwa na nchi nyingine duniani. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la kimataifa la Open Doors kupitia kitengo chake cha World Watch List kuanzia kipindi cha November 1, 2012 hadi Machi 31, 2014, Nigeria imeshika namba moja ikifuatiwa na mataifa ya Syria, Misri, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Mexico, Pakistan, Colombia, India, Kenya na Iraq.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo imeegemea takwimu za namna makanisa na mali za wakristo zilivyoteketezwa, na maasi dhidi yao mathalani kupigwa, utekwaji nyara, ubakaji, kukamatwa hovyo na hata kulazimishwa ndoa, inaonyesha kuwa Nigeria inaongoza ikiwa na matukio 2,073 huku Syria ikiwa na matukio 1,479. Mataifa mengine yanayofuatia ni pamoja na Jamhuri ya Afrika ya Kati 1,115, Pakistan 228, Misri 147, Kenya 85, Iraq 84, Mnyanmar (Burma) na Sudan ikiripotiwa kuw ana 33, na Venezuela ikiwa na matukio 26.

"Kujitangaza kwamba ni mkristo kwenye mataifa haya ni kama kujitoa mhanga, unajiweka hatarini"

Na kati ya mauaji 5,479 ya wakristo duniani kote, Nigeria, Syria na Jamhuri ya Afrika ya Kati wameunda asilimia 85 ya jumla hiyo, huku takwimu zikikadiria kuwa kuna wakristo 322 wanaouwawa kila mwezi.

Korea ya Kaskazini, taifa ambalo linaongoza kwa mateso ya wakristo kwa mwaka 2014, halijaorodheshwa kwenye 'kumi bora' kutokana na kinachoendelea nchini humo kuwa cha siri mno kiasi kwamba unaweza usijue kilichopo, kulinganisha na muundo wa utafiti huo ambao umebeza taarifa za mitandao, vyombo vya habari na maofisa walioko ngazi za chini kwenye jamii mbalimbali.

Ripoti ya utafiti huo ambayo inaonyesha namna mtu anayehusihwa na imani ya Ukristo anavyopata mateso yapatikana hapa. Unachoweza kufanya kwa ajili ya mataifa haya kwa dakika tano tu ni hiki hapa.

Taarifa fupi kutoka utafiti huo.

1. Nigeria;
Taifa hili limegawanyika katika maeneo mawili, kusini na kaskazini, ambapo kusini mwa nchi hiyo kumekaliwa na wakristo wengi, wakati huko kaskazini kuna idadi kubwa ya waislamu. Matukio mengi yameripotiwa kutokea eneo la kaskazini ambapo maeneo yake mengi yanatawaliwa na sheria za kiislamu, ambapo hata hivyo kundi la Boko Haram limejikita zaidi kuwabadili watu kuwa waislamu, wakishambulia wakristo silaha mbalimbali ikiwemo mabomu na hata utekaji nyara. Sababu nyingine inaelezwa kuwa ni uwepo wa kundi la kiislamu la Fulani (Muslim Fulani Herdsmen) ambao huvamia maeneo ya wakristo na kuwapora ardhi.


2. Syria;
Idadi ya wakristo nchini humu inaripotiwa kuwa chache, na katika kipindi cha kuandaliwa ripoti ya utafiti huu, ianoyesha kuwa wakristo wengi wameuwawa kutokana na vita inayoendelea nchini humo, msimamo wa waislamu wenye itikadi kali waliopo kwenye kamundi yanayoshiriki vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo na pia hata kuwekwa kati kwa wakristo baina ya makundi ya Shia na Sunni yanayohasimiana. Aidha wakristo wameendelea kuwa kwenye hatihati nchini humo kutokana na kukisiwa kuunga mkono utawala wa Bashar al-Assad.

3. Misri;
Taifa hili ambalo lipo kwenye mpito, lina idadi kubwa ya wakristo kwa mwamvuli wa kikoptiki (Coptic Orthodox Christians), linatatizwa na mashambulizi mbalimbali ambayo yalizidi kushamiri mara baada ya kuondolewa madarakani Rais Mohamed Morsi mnamo July 2013. Ambapo kikundi cha Muslim Brotherhood pamoja na makundi mengine yamehusika na mashambulizi hayo ikiwemo kuchoma makanisa na mali za wakristo nchini humo, na pia mauaji.
 
4. Jamhuri ya Afrika ya Kati;
Japokuwa taifa hili lina idadi kubwa ya wakristo kulinganisha na makundi mengine, ripoti inaonyesha kuwa kundi la Séléka limekuwa likilenga jamii ya wakristo, ikiwemo vijiji, ambapo lengo lao kuu ni kutaka kulibadili taifa hilo kuwa la kiislamu. Licha ya kwamba mateso yameripotiwa, matukio mengine huenda kuwa yameachwa kutokana na kutopata usahihi wa taarifa.

5. Mexico;
Ukabila na rushwa imeripotiwa kuwa chanzo kikuu cha mashambulizi kwa wakristo nchini humu, ambapo licha ya wingi wao, wakristo wamelazimika kuishi kwa mashaka kutokana na maeneo waliyopo kuongozwa na mila ambazo mtu akikengeuka huweza kushambuliwa. Na kundi kuu ambalo limekumbwa na athari hizi ni jamii ya Wapentekoste, Walutheri na pia 'Presbyterian'

Comments