SILAHA ZA VITA VYETU.

Na Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima.
Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe
 
Watu wengi hudhani kuwa kukariri maandiko mengi na kushika vifungu vingi vya biblia ndio uhakika wa kushinda vita; jambo ambalo si kweli!

Kufanya hivyo ni sawa na kusema kuwa ukinunua silaha nyingi za kivita ndio uhakika wa kushinda vita; lakini ukweli ni kuwa bila kujua jinsi ya kuzitumia unaweza kujikuta umeangamizwa kwa silaha zako mwenyewe.

Ni muhimu kujua jinsi ya kulitumia neno la Mungu katika vita ili upate ushindi mkamilifu. Tumepewa mamlaka ya kukanyanga nyoka na ng'e (luka 10:19) andiko hili haliwezi kutenda kazi mpaka umefahamu jinsi ya kuitumia mamlaka uliyopewa.

Ni maombi yangu Mungu akuongoze katika vita katika jina la Yesu; hakuna kumiliki bila kupigana maana hata shetani alitoka mbinguni baada ya vita (Ufunuo 12:7-11)

Songa mbele haijalishi unapitia magumu kiasi gani usikate tamaa; endelea kupambana kwa neno la Mungu ushindi upo!!!


Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe

Comments