Kila jambo lina mwanzo na mwisho wake, kama mwanadamu anazaliwa na
baadae anakufa, basi siku ya jana ilikuwa ndio siku ya mwisho wa tuzo la
BET. Wenye kuchaguliwa walichaguliwa na wakupigwa chini walipigwa
chini. Lakini Bwana Yesu Kristo hakuangushwa alizidi kutawala katika
tuzo hizi. Tunamshukuru mtumishi wa Mungu TAMELA MANN ambaye alishinda
katika tuzo hizi zinazofanyika kila mwaka zikishirikisha mataifa
mbalimbali. Katika
kipengele cha watu wa Mungu yaani Gospel kulikuwa na waimbaji watano
ambao ni kama wafuatao Donnie McClurkin, Erica Campbell, Hezekiah
Walker, Tamela Mann*WINNER na Tye Tribbett Kama
unavyojua katika mashindano lazima mmoja aibuke mshindi, basi Tamela
aliweza kuwa mkali kwa mavoko yakutisha na uimbaji wake kwa ujumla.
Kazi
ya Mungu ukifanya kwa asilimia zote kama vile unavyohakikisha tumbo
lako linakuwa limejaa na haliumizwi na njaa, Mungu aweza kukuinua tu
hata iweje.
Comments