TULIKUWA WANNE SASA TUPO WATATU NA MAMA YETU MJANE, ATOA MACHOZI MWINJILISTI SARAH MVUNGI


Inaumiza sana unapoona yule ulikuwa unampenda anapopotea na kutoonekana tena duniani. Hii imemkutana mtumishi wetu Sarah Mvungi baada ya kupotelewa na mdogo wake Maria Patrisia Mvungi mkoani Tanga hivi karibuni. Tunahitaji kumuombea sana Mwinjilisti Sarah Mvungi ili asiweze kuyumba katika huduma yake ya kumtumikia Mungu. Leo hii hawezi kupata huduma alizokuwa akizipata kwa mdogo wake kwa mawazo na hata kifedha.

Kushoto ni Mwinjilisti Sarah Mvungi

Hakika duniani tunapita na tunahitaji kukaa katika BWANA ili siku ya mwisho tukamuone Baba yetu mbinguni. Unatakiwa kukumbuka kuwa kila kunapopambazuka ndipo unakaribia kaburi lako kwahiyo unatakiwa kujiandaa kwa maisha ya huko mbinguni.

Jamani inaumiza sana kuona leo hii mama na Sarah Mvungi kuitwa mama wa marehemu Maria Patrisia Mvungi na kumbuka mama huyu ni mjane, labda Maria alikuwa faraja kwake, leo hii anakosa huduma ya Maria. Tumuombee sana mama yetu ili Mungu ampe uwezo wa kusahau na kutambua kuwa yako maisha mengine zaidi ya haya ya hapa duniani.

Comments