TUMEITWA ILI TUWE WANYENYEKEVU.

Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla
" Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; " Mathayo 11:29
Bwana Yesu asifiwe sana...
Ngoja tutafakari kidogoo,kuhusu hilo andiko hapo juu. Bwana Yesu anatualika twende kwake,kwanza kabisa tujitie NIRA yake...
Kwa wale wafugaji wanafahamu kwamba pingi ngo'mbe watakapo kulima wakiwa wawili,au zaidi,basi mchungaji hana budi ya kuwafunga kwa kuwaaunganisha kwa pamoja katika shingo zao kwa likitu kama chuma,kamba hivi,au kama mfano wa mbao fulani iliyotengenezwa rasmi Vyombo hivi ni NIRA kwa hao ngo'mbe.
Hivyo ngo'mbe hao huweza kulima kwa pamoja bila kuachana,na kutembea kwa pamoja bila kuachana.

NIRA ya Bwana Yesu ni nyepesi si kama hiyo ya mfano wa ngo'mbe. Nira ya Bwana Yesu hutufanya tuweze kutembea na Yeye kwa pamoja.
Yeye aliyefungiwa NIRA na Bwana Yesu huungamana naye,na mtu wa namna hiyo huongozwa na Bwana muda wote,wakati wote,sababu ya kufungiwa NIRA na Bwana Yesu.

Lakini pia katika andiko hilo tunaalikwa rasmi KUJIFUNZA KWAKE BWANA YESU,...kwa kuwa Yeye ni mpole na mnyenyekevu wa moyo.
Maisha ya Ukristo ni maisha ya kujifunza kwake Yesu siku zote,muda wote pasipo kuchoka. Ikiwa ndio hivyo basi,tunaye mwalimu MMOJA TU chini ya jua,naye ndiye BWANA YESU pekee.Ukimuona mtu ni mjuaji kwa habari ya maisha ya wokovu,basi mtu huyo ndiye asiyejua kuliko wote,maana kwake Yeye Bwana sisi tu wanafunzi siku zote za maisha yetu.
Sasa unisikilize mpendwa kwa makini;
Maisha ya mkristo ni maisha ya UNYENYEKEVU WA MOYO.

Ikiwa kama utabahatika kumuona mkristo mnyenyekevu wa moyo,basi huyo ndiye mkristo haswaa.
Shida kubwa siku ya leo,ni kutokuwa WANYENYEKEVU na ndio maana hatuvuki kiimani wala kimaendeleo.

Kinyume cha unyenyekevu ni KIBURI.
Sasa;
Kila mtu anakiburi,lakini si kila mtu ana unyenyekevu!
Umeipata hiyo,
Nasema hivi;
Kila mtu anakiburi,ila tunatofautiana viwango maana wengine viburi vyao huonekana sana kwa nje,wengine kiburi hujificha kwa ndani,lakini wanavyo.

Kila mwili wa mwanadamu hupenda kueshimiwa na kuonekana ni mzuri,bora kuliko mwingine kimawazo,kimaneno au hata kimatendo. Ile hali ya kujiona wewe ni bora sana kuliko wengine ni KIBURI.
Hakuna mwanadamu asiyependa kuheshimiwa,ila sasa tunatofautiana viwango.
UNYENYEKEVU ni kinyume cha kiburi,maana yake ni kujishusha hadi viwango vya chini,kuwaona wenzako ni bora kuliko wewe.
Leo hii Bwana Yesu anatutaka sisi tulio ndani yake,tuwe na UNYENYEKEVU WA MOYO maana hapo ndipo ukristo wetu upo.
Ukristo haupo kwa kujiita kwamba " mimi ni mkristo,nimeokoka nampenda Bwana Yesu " wala kujiita majina makubwa katika utumishi mara " Apostle,mchungaji,Mwalimu.N.K " BALI UKRISTO WETU HUPIMWA NA MOYO WA UNYENYEKEVU,BAADA YA KUOKOKA.

Hakuna aliyekuwa mnyenyekevu wa kwanza na wa ukweli kama BWANA YESU KRISTO na ndio maana tunasoma;
" tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; "Wafilipi 2:8-9

Haleluya...
Hata jina la Bwana Yesu lilipotolewa, limetolewa kwa sababu ya unyenyekevu alionao.
Hivi unafikiri kwamba Bwana Yesu alishindwa kushusha moto kutoka mbinguni awateketeze wote waliokuja kumkamata,hata wale waliokuwa kinyume nao?

JIBU;
Alikuwa anaweza kufanya hivyo.
Lakini kwa kuwa alikuwa MNYENYEKEVU WA MOYO ili litimie neno la Bwana,ya kwamba mwana wa adamu atateswa,atasulibiwa na siku ya tatu atafufuka.

Bwana Yesu asifiwe...
Ukitaka unyanyuliwe,basi ujishushe.
Tazama tu,kwa haraka haraka,mtu yule atakaye kujenga ghorofa ndefu,basi ni lazima msingi wake ushuke chini sana.
Ukitaka ghorofa iende juu,basi msingi huna budi kushuka chini zaidi,na hivi ndivyo ilivyo hata kwako. Ukitaka Bwana akuinue basi ushuke chini zaidi,na kushuka chini zaidi ndio UNYENYEKEVU wenyewe.

Bwana Yesu asifiwe sana,...
Biblia inatuambia tukijifunza kwake;jambo moja analotuambia Bwana baada ya kujifunza kwake,ni kwamba;
" ;..nanyi mtapata raha nafsini mwenu; " Mathayo 11:29

Kumbe ipo raha halisi ipatikanayo ndani ya Yesu Kristo. Raha hii haifanani na raha zozote zile,na hata ukiniambia nikuelezee ni raha ya namna gani,wala siwezi kukuelezea,ila jambo moja ninaloweza kukuambia ni kwamba NJOO KWA YESU KRISTO,KISHA UONE RAHA IPATIKANAYO.
* Kwa huduma ya maombi na maombezi,usisite kunipigia katika namba yangu hii;
0655111149.

UBARIKIWE.

Comments