TUMIA VIZURI MIAKA NA BARAKA AMBAZO MUNGU AMEKUJALIA KUPATA.


BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.

Karibu tujifunze jambo la muhimu la kuhusu miaka na Baraka ambazo MUNGU anatupa.

Waamuzi 17:1-13 ( Wakati huo alikuwako mtu mmoja wa nchi ya vilima ya Efraimu, ambaye jina lake alikuwa akiitwa Mika. .........................Mama yake akasema, Mimi naziweka fedha hizi kabisa ziwe wakfu kwa BWANA, zitoke mkononi mwangu kwa ajili ya mwanangu, ili kufanya sanamu ya kuchonga, na sanamu ya kusubu; basi kwa hiyo nakurudishia wewe.  Basi hapo alipomrudishia mama yake hizo fedha, mama yake akatwaa fedha mia mbili, akampa fundi mwenye kusubu fedha, naye akafanya sanamu ya kuchonga kwazo, na sanamu ya kusubu; ambazo zilikuwa ndani ya nyumba ya Mika.  Basi mtu huyo Mika alikuwa na nyumba ya miungu, naye akafanya naivera, na kinyago, akamweka wakfu mmoja miongoni mwa wanawe, akawa kuhani wake.   ).

Ndugu yangu unaitumiaje miaka yako ya kuishi?

MUNGU alimpa Mika vitu vingi lakini Mika alivitumia vibaya.

Kuna njia unawaza kuiendea lakini ikawa sio nzuri.

Miaka ya Mika aliitumia vibaya wakiwa na mama yake maana kwa miaka kadhaa aliyumika kama kuhani wa miungu.

Mika alimwibia mama yake  na tena hata baada ya hapo mika aliendelea kutumia vibaya miaka yake maana aliitumikia miungu.

Mama yake na mika alimtumia mika katika ibada ya shetani, Ndugu yangu usikubali mtu yeyote akakutumia katika mambo yake ya kipepo maana utaitumia vibaya miaka yako.

Zaburi 90:12 (Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima. ).

Unaitumiaje miaka yako ya kuishi?

Unaitumiaje miaka yako ya kukaa Tanzania kama wewe mteule wa KRISTO?

Unaitumiaje miaka yako ya kukaa Kenya au Uganda wewe mteule wa BWANA YESU?

Unaitumiaje miaka yako ya kukaa Kongo au Rwanda au Burundi au Ulaya wewe mteule wa KRISTO?

MUNGU anatufundisha kuitumia vizuri miaka yetu. Mwanzo 5:25-27 ( Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi. Mahalaleli akaishi baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa. )

Methusela aliishi miaka mingi kuliko wanadamu wote  lakini miaka yake aliitumia sio kwa utumishi mzuri kwa MUNGU. Historia yake inazungumzia tu kuoa na kuzaa watoto.

-Ukiitumia vibaya miaka yako utasababisha  hasara kubwa kwako na kwa ndugu zako.

- MUNGU akulinde miaka yako yote na uache habari njema ambayo itakuwa mfano kwa wengine kwa miaka mingi ijayo.

Waamuzi 18:27-31 ( Nao wakakitwaa hicho alichokuwa amekifanya Mika, na kuhani aliyekuwa naye nao wakafikilia Laisha, kwenye watu waliokuwa wenye starehe na hifadhi, wakawapiga kwa makali ya upanga; wakaupiga moto mji wao. Wala hakuwako mwokozi, kwa sababu huo mji ulikuwa ni mbali sana na Sidoni, nao hawakuwa na shughuli na mtu awaye yote; na mji huo ulikuwa katika hilo bonde lililo karibu na Bethrehobu. Nao wakaujenga huo mji na kukaa humo. Wakauita mji jina lake Dani, kwa kuliandama jina la baba yao Dani, aliyezaliwa kwake Israeli; lakini jina la mji huo hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Laisha. Kisha wana wa Dani wakajisimamishia hiyo sanamu ya kuchonga; na Yonathani mwana wa Gershomu, mwana wa Musa, yeye na wanawe walikuwa ni makuhani katika kabila ya Wadani hata siku ya kuchukuliwa mateka hiyo nchi. Basi wakajisimamishia hiyo sanamu ya kuchonga aliyoifanya Mika, wakati wote ile nyumba ya MUNGU ilipokuwako huko Shilo. ).

Hapa tunaona hasara mbaya sana ambayo ilisababishwa na Mika.

-Fanya kitu ambacho kitamletea hasara shetani na sio faida.
 Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           +255714252292

                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments