TUNATAKIWA TUWE NA MAOMBI YA KUKESHA.



 
BWANA YESU asifiwe.

Leo tunazungumzia Maombi ya kukesha.

Maombi ni mkono mrefu wa kupokea kile ukitakacho kutoka kwa MUNGU.

Kukesha maana yake ni kudumu.

Maombi lazima yawe na mkesha au kukesha pia mkesha lazima uwe na maombi.

Mkristo anatakiwa awe na maombi ya kukesha na anatakiwa adumu katika maombi miaka yake yote.

Mtu anavuna alichopanda, ukipanda kwa maombi ya mkesha utapokea.

Zaburi 91:15-16( Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza; Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu. ).

-Huwezi kuitika kama hujaitwa na MUNGU hawezi kukuitikia kama hujamwita.

-Tunamwita MUNGU katika maombi na tunapaswa tumwite siku zote, Ndipo hata uhusiano wetu na MUNGU utakuwa imara.

-Mitume walimwita MUNGU akawaitikia.

-Manabii walimwita MUNGU akawaitikia.

-Hata wewe unaweza ukamwita MUNGU leo na ukapokea ila uwe na  nia ya kweli.

 Nia ya kweli ni ipi? Mathayo 6:5 ( Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. )

                           1.  Kutokupayuka  payuka.

                          2.   Kutojionyesha kwa watu.

Luka 11:11-13( Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka? Au akimwomba yai, atampa nge? ).


-Tuombe maombi tukiwa watakatifu.

-Tuombe tukiwa wasafi wa mioyo.

-Tuombe tukiwa katika KRISTO YESU na MUNGU atajibu maombi.



Tuwe waaminifu wa kweli kwa BWANA. Zaburi 55:16-17 (Nami nitamwita MUNGU, Na BWANA ataniokoa;  Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu. ).

Ndugu yangu usiende kanisani kuomba tu bali na kukesha.

Zaburi 34:1-4 (Nitamhimidi BWANA kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima. Katika BWANA nafsi yangu itajisifu, Wanyenyekevu wasikie wakafurahi.  Mtukuzeni BWANA pamoja nami, Na tuliadhimishe jina lake pamoja. Nalimtafuta BWANA akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote. ).

BWANA YESU asifiwe.

Maombi ya kukesha ndio maombi yatakayokuzingira siku zote dhidi ya kila mpango wa giza, utafika ambako wengine hawawezi kufika.

Omba kwa kukesha  na katika maombi yako siku zote omba kwa imani maana pasipo imani huwezi kupokea.

Luka 21:36( Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu. ).

Maombi ni maisha.
  Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292

                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments