UNAMFAHAMU SHUJAA WA MSALABA?


Haleluya watu wa MUNGU.
Leo nina ujumbe wa kipekee sana na ambao hakika ukijifunza na kuzingatia hautabaki kama ulivyokua kabla hujajifunza.
Nazungumzia SHUJAA WA MSALABA.
Msalaba maana yake ni mateso.

Tunaye shujaa mmoja tu aliyepaingia patakatifu ili kutupa uzima wetu.
Huwezi kuwa shujaa kama hukupambana na kushinda.
Huyu shujaa ninayemzungumzia ni shujaa wa mashujaa maana alishinda kwenye kila shindano.

-Penda kutembea ukiwa na shujaa sio kutembea na aliyeshindwa.
-Shujaa ana mbinu za ushindi.
-Shujaa ana sifa za ushindi.
-Shujaa ana sifa za ushindi.
-Ukiwa na shujaa huyu utaishi Maisha ya Ushindi
Tunamzungumzia shujaa wa msalaba maana yake ni shujaa wa mateso.
Msalaba ni mateso lakini yuko shujaa wa mateso.
Kwanza yeye alishinda ndio maana ana sababu za kukushindia na wewe unayepitia kwenye mateso.
Ufunuo 5:1-10 ( Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba.  Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake?  Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.  Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.  Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye AMESHINDA apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.  Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za MUNGU zilizotumwa katika dunia yote.  Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi.  Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu. Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia MUNGU kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa MUNGU wetu; nao wanamiliki juu ya nchi. ).

Mambo haya Yohana aliyashuhudia akiwa mbinguni.
Shujaa huyu ni BWANA YESU KRISTO, yeye alishinda ila akushindie na wewe.
-        YESU ni shujaa wa magonjwa maana nguvu zake zikishuka kwenye ugonjwa  uzima unaingia.
-        YESU hakopeshi, ukimwambia atende anatenda.
-        YESU hachelewi, hakawii wala hawahi ila kwa wakati wake anatenda.
-        Tunaye shujaa wa msalaba ambaye udhaifu wetu wote aliuweka msalabani na kuuacha pale.
-        Malaika mbinguni walimsujudia yeye, Wazee 24  walimsujudia kwa sababu yeye ni shujaa wa masalaba.
-        YESU haaibiki wala haaibishi
-        Huwezi kuitwa shujaa kama hujashinda popote.
-        YESU ni shujaa wa mashujaa wote.
‘’Tanzania huwa tunasherekea siku ya mashujaa kwa sababu mashujaa hawa walitoa uhai wao kwa ajili ya ukombozi wa Msumbiji na kwingineko. Hawa hakika ni mashujaa na wanaitwa mashujaa baada ya kushinda’’ Lakini yuko YESU KRISTO  shujaa wa masalaba ambaye yuko tayari kukushindia katika jaribu lako, tabu yako, shida yako na matatizo yako.
Tuwe radhi kumwendea shujaa wa masalaba  wa uzima kwa ujasiri.
Shujaa wa masalaba yuk oleo hapo hapo ulipo yeye anasubiri tu  aone unamwomba nini.

Ukikaa kimya wewe huna hitaji lakini ukiwa na hitaji kama Bartimayo unaomba. Luka 18:40-43 ( Basi wale waliotangulia wakamkemea ili anyamaze; lakini yeye alizidi sana kupaza sauti, Ee Mwana wa Daudi, unirehemu. YESU akasimama, akaamuru aletwe kwake; na alipomkaribia, alimwuliza, Wataka nikufanyie nini? Akasema, BWANA, nipate kuona. YESU akamwambia, Upewe kuona; imani yako imekuponya. Mara hiyo akapata kuona, akamfuata, huku akimtukuza MUNGU. Na watu wote walipoona hayo walimsifu MUNGU. ).
Bartimayo alikuwa na msalaba wake yaani mateso yake kwa miaka mimi. Kwa mateso yake hayo yawezekana alikuwa hajawahi hata kuwaza kama atakuja siku moja akapata mchumba na kuchumbia na hatimaye kufunga ndoa takatifu . Alikua na mateso motoni lakini alipokutana na Shujaa wa msalaba alimponya. Baada ya Bartimayo kuelewa shinda yake alipona, je wewe una shida gani ambayo unataka shujaa wa msalaba akuponye?
Watu walimwambia Bartimayo ‘’Wewe kipofu usimsumbue mheshimiwa, baki hapa sisi twende maana mheshimiwa hugeuza  mkate mmoja kuwa mikate mingi tunakula na kushiba, wewe mchafu baki hapa’’
Lakini Bartimayo aliendelea kumtumainia Shujaa wa msalaba  na hakika alipona. Ndugu yangu  yawezekana  watu wanakudharau  kwa sababu ya kwenda kwako kwenye maombi. Ndugu yangu nakuomba ng’ang’ania tena ng’ang’ania hakika utapokea. Shujaa wa msalaba anajua teso lako maana hata yeye aliyapitia hayo lakini aliyashinda.
Hitaji la Bartimayo ni la muhimu sana kwa YESU ndio maana alimwita na akamponya.Hitaji lako ni la muhimu sana kwa YESU kama ilikuwa kwa Bartimayo.

Yohana 14:14-15 (Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Mkinipenda, mtazishika amri zangu. )
Wema wa MUNGU haupungui popote; Yeye anafanya chochote kwa yeyote hata kama ni kilema, kipofu , kiwete na hata ni mkoma kama naamani.

SHUJAA WA MSALABA NI BWANA YESU NA ANAWEZA YOTE .
 Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292

                 MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

 MUNGU Akubariki.

Comments