Unawaza nini juu ya Bwana?



Maombi ni silaha ya kila mkristo.

Kitabu cha Nahumu sura 1:9, inasema unawaza  nini juu ya  Bwana?
Yeye ambaye anaweza kukomesha mateso tunayopitia.

Mpendwa mwana wa Mungu yako mambo mengi  tumekuwa tukiomba na kulia mbele za Mungu, bila kupata majibu. Leo hii Mungu anauliza  unawaza nini juu yake? Hili ni swali gumu lakini kwa mtu aliye Rohoni ni jepesi sana.
Ø  Kila mtu aliyeumbwa kwa sura na  mfano wa Mungu, tambua kuwa kuna vitu vya thamani ndani yako, ambavyo ni vipawa na karama. Na Mungu leo anataka uvitumie hivyo katika kuujenga ufalme wake ili akuinue na kukupatia yale mahitaji unayoyaomba kwake. Maana maandiko yanasema utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na mengine yote mtazidishiwa.
Ø  Mwana wa Mungu haijalishi kwamba unapitia magumu kiasi gani au uko katika mazingira gani?
Mungu anataka akutumie ili uubadilishe huu ulimwengu. Usijidharau hajalishi kuwa wewe ni :-
 -Mzee
- Mtoto
-Haujasoma  au ni masikini Mungu anataka akutumie vile ulivyo.

Ø  Tukimwangalia nabiiYeremia katika kitabu kile cha Yeremia sura 1:1……………..
Yeremia yeye alikuwa anajitetea kuwa ni mtoto lakini Mungu alimwambia kuwa ataweka maneno katika kinywa chake, na kumpatia uweza wakung’oa, kubomoa na kuharibu.
Ø  Mungu anaangalia mtu aliyeko tayari ili amtumie. Ni mara ngapi Mungu amesema na wewe lakini unatoa uzuru? Ondoa hofu, woga, kutokujiamini ili Mungu akutumie.

Ø  Mungu anapokupa maono wewe usisite wala usiangalie kwamba huna pesa au haujasoma Chukua hatua na Mungu atainua watu wa kuyategemeza hayo maono.
Tukiangalia katika kitabu cha Nehemia 2:1…………, tunaona jinsi Mungu alivyompa Nehemia Maono ya kuujenga ukuta ule wa Yerusalemu, Nehemia baada ya Mungu kusema naye alibeba mzigo wa yale maono kasha akafunga na kuomba na Mungu akamwinulia watu wakuifanikisha ile kazi ya kuujenga ukuta wa Yerusalemu.

Ø  Tumeomba miaka mingi , tumefunga, lakini bado hatujajibiwa haja zetu, wengine tunaomba,
Wenzi wa maisha,   watoto,  ndoa zetu kupona, kuinuliwa uchumi,  biashara zetu kuongezeka,kuponywa magonjwa nk. Lakini bado hivi vyote havijatimia, hatatumefikiahatuayakumlaumuMungu,nakudhanikuwaanaubaguzi la hasha! Mungu anataka ufanye ya kwake na yeye afanye ya kwako.

Ø  Wengine tunajisifia tumeokoka siku nyingi tunasema tuna miaka ishirini ya mwokovu, lakini hatujaweza kufanya kitu chochote kwenye ufalme wa Mungu. Hata kumshuhudia mtu mmoja hatujawahi? Wako watu wagonjwa wamekosa tumaini, wako walevi wako makahaba, usiache wakafia dhambini,Unasubiriwa wewe ufungue kinywa chako useme neno ili waweze kuwekwa huru.
( Yohana 12: 26)  inasema mtu akinitumikia na anifuate name nilipo na mtumishi wangu atakuwepo. Tena mtu akinitumikia  baba  atamheshimu.

Jina la Yesu libarikiwe

Haleluyaa, mtumikie Mungu ili na yeye akutumikie.
Amen.

 E Lyimo.
Cell: 0756 496 496

Comments