USHUHUDA: NILIFAULU MITIHANI KWA UDANGANYIFU


13186089-3d-render-of-man-carrying-book-on-his-back-concept-of-learning-difficulties
Sikupata maksi nzuri kwenye mitihani yangu pale nilipohitimu elimu ya
sekondari. Nilirudia mitihani mara mbili zaidi lakini bado sikupata maksi nzuri.
Ndipo rafiki yangu mmoja alinishauri nijiunge na Chuo cha Taifa cha Ualimu.Ilikuwa ni kozi ya miaka miwili. Sasa ninatambua kuwa kile nilichofanya wakati wa mitihani hakikuwa kizuri

…Usidanganye!
Kabla ya mitihani kuanza, Mungu aliniambia mara kadhaa kwenye mawazo
yangu, “Usidanganye”. Lakini sikusikiliza kwa sababu nilijua haikuwa rahisi kwa mimi
kupata maksi nzuri kwenye mitihani. Sikudanganya kwenye mtihani wa kwanza, lakini baada ya hapo, niliingia na kidaftari changu kwenye chumba cha mtihani. Nilinakili majibu kutoka humo. Hivyo, nikafaulu mitihani kwa maksi nzuri sana. Nilifahamu moyoni mwangu kuwa ni makosa. Nilijisikia hatia na aibu.
Nilimwomba Mungu msamaha. Nilidhani hiki tu ndicho nilichotakiwa kufanya. Kwa
hiyo, nilitumia maksi zangu nzuri kuendelea na masomo zaidi. Niliweza kwenda Chuo cha Ualimu cha Kwara. Nilienda kwenye masomo, lakini sikuwa na amani moyoni.
Mawazo yalinijia, “Umefanya makosa. Matokeo haya si yako.”Kisha nilijiambia,
“Nimemwomba Mungu msamaha, hiyo inatosha.”Lakini mawazo haya hayakunipa amani kabisa.

Niliomba msaada
Hatimaye nilienda kwa viongozi wangu wa kanisa ili kuomba msaada. Waliniambia
kuwa haitoshi tu kumwambia Mungu nisamehe. Ni lazima nionyeshe toba yangu kwa kuweka sawa mambo niliyokosea. Kwa upande wangu, hiyo ilimaanisha kumweleza mkuu wa chuo kuwa nilikuwa nikidanganya kwenye mitihani. Hivyo, sikustahili kuingia chuoni. Niliandikia barua na kumweleza mkuu wa chuo yale niliyoyafanya. Niliipeleka barua ile ofisini na kumpatia katibu muhtasi wake. Katibu aliisoma barua ile. “Barua hii ikimfikia mkuu wa chuo, utapelekwa gerezani,”alisema. Hii iliniogopesha sana. Kisha katibu yule akasema, “Rudi nayo ukatafakari zaidi.”
Mshangao!
Nilirudi tena kwa viongozi wa kanisa na kuwaeleza alichoniambia katibu muhtasi.
Wakasema bado inanilazimu niende kwa mkuu wa chuo. Hivyo, siku iliyofuata nilienda
tena. Nilimwona kwanza katibu na kumwambia,“Nahitaji kumwona mkuu wa chuo.” Akanipeleka kwake. Unajua, mkuu wa chuo alikuwa mwema kwangu. Aliniambia nisiogope bali nimwendee aliyekuwa msimamizi wa mitihani, kisha nikamweleze kile ambacho nilifanya. Nilipoenda, yule msimamizi naye aliniruhusu nifanye mitihani tena. Nilifaulu! Hivi sasa nimerudi tena chuoni, lakini cha muhimu zaidi, Mungu ameniondolea hatia na nina amani moyoni mwangu.

Lawrence kutoka Nigeria. Ilimbidi ajifunze somo kuhusu
kufanya mitihani: si vizuri kudanganya. Lakini pia alijifunza kuwa haitoshi tu
kusema ‘samahani’. Ni lazima tujaribu kusahihisha makosa tuliyofanya.

Je wewe umefanya makosa gani na je unaweza chukua hatua sasa kama Lawrence?

Comments