USIWE MWEPESI WA KUSEMA AMEN.



Neno Ameen; ni neno dogo lakini lina maana kubwa sana! Lina uwezo wa kubeba mjumuisho wa ma maneno Elfu elfu

Maana yake; NA IWE, (IMEKUWA)

Sasa basi imekuwa ni kawaida kwa watu wengi kukosea (typing error) hata mimi pia huwa nakoseaga!

Mfano;
Utakuta mtu ameandika;
"mungu akubariki utokapo na uingiapo, mungu akubariki katika kazi za mikono yako, mungu akufanye kichwa wala sio mkia, mungu awapige maadui zako mbele zako nk
Kumb 28:2-7"

Na wengine wameweka picha flani flani wakifananisha na Yesu huku wakiwa wameambatanisha na ushuhuda flani hivi

Halafu anakutarget(anakwambia) Sema(Type) Ameen!

Na sisi bila kujua tunasema Ameen!

Wapendwa katika Kristo; kuna tofauti kubwa kati ya mungu wa herufi ndogo na Mungu wa herufi kubwa! Unaposema Ameen kwa mtu akiyemtaja mungu kwa herufi ndugu maana yake umemwitikia Shetani moja kwa moja katika ulimwengu wa Roho!

Hebu soma hapa upate kuona tofauti ya mungu wa dunia hii na Mungu muumba mbingu na nchi! 2kor 4:3-5

Tuwe makini wapendwa wng, na tuwe teyari kurekebishwa, kwa utukufu wa Mungu! Binafsi napenda kurekebishwa na kufundishwa pia maana najua kuwa bado sijajua vile inipasavyo kujua!

TUACHE UNAFKI;
Mtu akiona ni rafiki yake amekosea typing error! Hasubutu kumrekebisha, kwa kumuonea haya! Au kuogopa kumkwaza nk! Lakini kumbuka rafiki yangu, hiyo nayo ni Injili! Na neno linasema yeyote atakayeionea haya Injili mimi (YESU) nami nitamwonea haya mbele ya Baba yangu! Hivyo kuwa makini ndugu yangu! Turekebishane kwa UPENDO.

Mungu awabariki sana sana!
Saloom Shaloom.

By Lucy Marandu.
hii imetoka facebook.

Comments