VIPINDI VITATU VYA SAFARI YA NDOA.



1. MUME NA MKE WAWILI TU KATIKA NDOA KABLA YA KUPATA WATOTO - MIAKA 3 YA KWANZA

2. KIPINDI CHA KUZAA WATOTO NA KUKUZA WATOTO - MIAKA 25 - 35

3. KIPINDI CHA MWISHO MUME NA MKE WAWILI TU, WAKATI WATOTO WOTE WAMESHAONDOKA KATIKA HIMAYA YA WAZAZI

KIPINDI CHA KWANZA
MUME NA MKE WAWILI TU KATIKA NDOA KABLA YA KUPATA WATOTO - MIAKA 3 YA KWANZA

1. Hiki ni kipindi muhimu sana katika kujenga msingi wa ndoa.

2. Ni kipindi muhimu kwa wanandoa kufurahiana na kujuana.

3. Ndio kipindi ambacho wanandoa hufurahia tendo la ndoa kuliko kipindi kingine chochote.

4. Kwa ushauri wa kitaalamu inapaswa wananoa wakae angalau miaka katika kipindi hiki kabla ya kupata mtoto.

5. Kwa bahati mbaya wanandoa wengi wakisha oana tu, haraka sana wananaza kupata mimba na kufanya kipindi cha kufurahia tendo la ndoa kuwa kifupi sana.

6. Wakati mwingine mila na destuli zimechangia sana kuharakisha wanandoa wachanga kupata mtoto mara tu baada ya kuoana.

7. Wengine siku ile ile ya kwanza ya kukutana tayari na mimba inapatikana siku hiyo hiyo hii sio afya kabisa kwa ndoa.

8. Wanandoa wapate muda wa kuwa wawili kwanza kwa miaka michache ya mwanzoni. Kisha baada ya hapo waanze kufikiria swala la kupata watoto.

9. Nawashauri vijana ambao hawajaoa bado na waliooa hivi karibuni wasiwe na haraka ya kukimbilia kutafuta mtoto kwanza wawe na muda wa kutosha wa kufurahiana kabla safari ya kulea watoto haijafika.
MUNGU akubariki sana na kama hukusoma sehemu ya pili ya somo hili ambayo ilikuja mapema kabla ya sehemu ya kwanza FUNGUA HAPA
Mchungaji Peter Mitimingi katika moja ya semina za wanandoa, hapa akifundisha wanandoa.

Comments