WAIMBAJI WA INJILI WOTE SOMENI HII.


BWANA YESU asifiwe.

Nawapenda sana waimbaji wa nyimbo za Injili, kwani wamekuwa wakimwadhimisha MUNGU kwa sauti zao!

Lakini pia nawasikitikia sana, waimbaji wa Nyimbo za Injili kwani wamekamata taasisi Muhimu sana AMBAYO lucifer ALIIONGOZA HUKO MBINGUNI kabla ya kutupwa Duniani!

Hivyo hakuna mtakachoweza kumdanyanya Lucifer kwa namna yoyote ile! Labda...

Muwe mbali na TAMAA
Muwe mbali na KIBURI
Muwe mbali na tabia ya KUJIINUA!
Muwe mbali na UDUNIA n.k

NA HUU NI UCHUNGUZI (MTAZAMO)WANGU BINAFSI, hivyo usinihukumu!

'Baadhi ya waimbaji wa nyimbo za Injili wana tabia za Ki-lucifer lucifer  Na tabia hii inaanza kidogo kidogo kama vile vile Lucifer alivyo anza kule mbinguni!'
Eze 28:13-19

Mwimbaji wa nyimbo za Injili anavyo anza, Ni mnyenyekevu ajabu! Lakini ngoja ajue ana sauti nzuri, au anawabariki wengi dah dah dah... ni balaa! yaaani ni shida! Hapo ndipo kiburi kinapoanzia!(kile kile cha Lucifer)

Hataki kurudiwa/kuonywa wala nini! Na ikiwa utamfuatilia fuatilia ndo mwanzo wa kuacha kwaya babisa nk!

Na wengine wakishaona wamesifiwa kuwa wana sauti nzuri au wana kipaji cha kipekee anaanza ubinafsi, muda kidogo kwenye kwaya za Kanisa na Muda mwingi wanatunga nyimbo zao binafsi kwa madai eti kuwafikie watu wengi zaidi!! Ha ha haaaa (Yale yale ya Lucifer)

Ngoja basi wawafikie hao watu wengi wanaodai.....
Majina yanabadilika mara utasikia:-
MALKIA WA NYIMBO ZA INJILI
STAR WA NYIMBO ZA INJILI
MSANII WA NYIMBO ZA INJILI
HIP POP WA NYIMBO ZA INJILI
TAARABU LA YESU
SEBENE LA UHAKIKA KWA YESU nk

Kimsingi nikiyaangalia haya majina Mmmmmh.... yana u..... ndani yake (SAMAHANI LAKINI)

Ukitaka kugundua hilo, we wacheki tuu hao jamaa wako bize na kuimba wala hawana Muda wa kuja kanisani kusikiliza neno la Mungu! wako bize na mialiko huku na huko!

Wanajifanya wanajua sana neno la Mungu hata wamesahau kuwa HAWAJAJUA VILE IWAPASAVYO KUJUA

Ukiongea nao wanasema "NIPO TAYARI KWA MIALIKO"

Sasa unamwalika Jumapili aje kuhudumu (kuimba), ajapo anasema naomba niwe wa kwanza kuimba kwani kuna sehemu nawahi! Hee hii ni ajabu, sasa huyu mtu amekuja kumwadhimisha nani sasa? Ikiwa ni YESU BWANA MKUBWA Mbona hataki kumsikiliza Boss wake(MUNGU) anasema nini?? Ina maana yeye alikuja kutumbuiza au kusifu katika Roho?? Kumbuka Kanisani kwake hajahudhuria Ibada huku alikopata mwaliko nako hataki kusikiliza neno! Inasikitika Mnoo!

Tuwe na busara wakati wote,(TUMFUATE YESU AMBAYE NI KIELELEZO CHETU)
Marko 1:35-39
Tunamwona Simon na wenzie wanamwendea Yesu wakimwambia; Watu wote wanakutafuta, lakini Yesu anasema Twendeni mahali Pengine, Hatuoni Yesu anashikamana na mambo mawili kwa wakati mmoja,aliamua kuwaacha wale akaenda mahali pengine! Na wewe ukiamua unaenda kuhudumu mahali, tulia umsikilize Mungu anasema nini mahali pale na siyo kuruka ruka tuuu huku na kule(MTAKA YOTE HUKOSA YOTE) Kauli za wahenga hizo.

Wengine wanauliza kabisa kuna Tsh.  ngapi ili nije kuimbaa?? Kwa madai eti watakujaje pasipo kupelekwaa?? Rumi 10:15
Ni kweli kuwa ikiwa mtaenda kuimba live kuna gharama usafirishaji wa vyombo n.k l.kini sii kwa dizaini hiyo wapendwa wangu! Ni bora mkamruhusu Roho wa Neema awajalie hekima zaidi!(Mpeni Roho Mtakatifu nafasi ili awape mwongozo katika yote muyaendeayo, acheni kutumia akili zenu zilizojaa njaa njaa)
Ni rahisi kupotea kama Lucifer, Jirekebisheni maana ile njia ni nyembamba mmno! Mt 7:21-27.

Mungu awabariki Waimbaji wa Nyimbo za Injili! NAWAPENDA SASA SANA!

Shaloom Shaloom!

By Lucy Marandu.

Comments