Hivi karibuni tuliona na kusoma katika mitandao na magazetini kuhusiana
na kifungo cha miezi mitatu jela cha mwimbaji wa nyimbo za injili
Tanzania Happy Kamili, lakini Mungu aliweza kumsimamia na kumtetea na
sasa yuko huru na anatumikia kifungo cha nje. Mwimbaji huu alituhumiwa
na kusomewa kifungo jela kutokana na kusababisha ajali barabarani.

Kutoka kulia ni Mess Jacob Chengula, Stella Joel, Happy Kamili na Ann Annie
Baadhi ya waimbaji wa nyimbo za Injili waliweza kufika nyumbani kwake na kumjulia hali na pia kumpa pole na kumpongeza kwa ushindi aliopata. Hakika hawa waimbaji wa nyimbo za Injili wanazidi kuonyesha upendo walionao na ushirikiano mzuri wakati wa shida na raha.
Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kimekuwa bega kwa bega kuhakikisha kazi na haki za waimbaji zinalindwa na pia kuhamasisha watu kuwa na ushirikiano na wenye kupendana wakati wa shida na raha.

MUNGU akubariki na kwa habari ya kwanza ya hukumu ni hii FUNGUA HAPA
Comments