WOKOVU KWANZA *sehemu ya mwisho *

Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


" Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu.
Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. " Luka 19:9-10

Maisha ya wokovu ni kuonana na Yesu na wala si vinginevyo. Hakuna maisha ya kumpendeza Mungu kama maisha ya wokovu. Vitu vyote chini ya jua havina maana kama kumpata Yesu wa Nazareti.

Yesu Kristo anamwambia Zakayo kwamba,wokovu umeingia nyumbani mwake,kwa sababu Zakayo naye ni mwana wa Ibrahimu,kwa lugha nyingine;
Yesu anasema,wokovu umeingia nyumbani mwa Zakayo kwa sababu Zakayo anastahili kuokolewa.

Hata sasa ninapohubiri katika madhabahu hii,ninakuambia kwamba wokovu umeingia nyumbani mwako,maana hata wewe unastahili.

Nami naamini kabisa,kupitia mfululizo huu wa fundisho hili kuanzia sehemu ya kwanza hata sasa,utafanya maamuzi ya kumpa Bwana Yesu maisha yako wewe ambaye bado hujaokoka, na hata wewe uliyeokoka,utafanya maamuzi ya kugeuka kwa kumtizama Bwana Yesu kwa mtizamo mwingine mbali na huo uliokuwa nao,kwamba IMANI yako iongezeke mara dufu.

Bwana Yesu asifiwe....
Haleluya,haleluya....

Zakayo aliyekuwa mtu mkubwa katika wotoza ushuru,mara tu alipoonana na Bwana Yesu,historia ya maisha yake ikabadilishwa. Akawa si Zakayo yule wa kwanza,maana hakuna mtu aliyekutana na Bwana Yesu kwa kufungua moyo wake,kisha akabakia vile vile alivyo.
Sababu ndani ya Yesu, kuna uzima kuna kuhuishwa tena,ngoja tuangalie andiko hili wakati tukiwa tunaendelea;

" Na tazama, wakaja watu wanamchukua kitandani mtu mwenye kupooza; wakataka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake.
Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampisha katika matofali ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya Yesu. Naye alipoiona imani yao, alimwambia, Ee rafiki, umesamehewa dhambi zako. " Luka 5:18-20

Tazama hapo,yule mgonjwa aliponywa mara alipofikishwa kwa Bwana Yesu,wala hakubaki na ugonjwa wake. Ndio maana ninakuhakikishia kwamba yeye amuendeaye Bwana Yesu,hupokea uponyaji wake. Hajalishi itachukua muda gani wa kudhihilisha uponyaji wako,lakini utapokea tu.

Lakini jambo moja la msingi tunalojifunza kwa andiko hilo ( Luka 5:18-20) ni hili;
• Kile kilichosababisha mgonjwa apokee uponyaji ni IMANI.
Maana biblia inasema ;
" Naye alipoiona imani yao,....... " Luka 5:20
Bwana Yesu hakumuona mgonjwa kama mgonjwa bali,alichokiona ni IMANI.

Ok,fanya hivi;
chukulia suala hili katika hali ya kawaida kabisa,kwamba Yesu kaletewa mgonjwa kitu cha kwanza kukiona inge'kuwa ni mgonjwa maana ndiye aliyeletewa. Lakini sasa Bwana Yesu hakumuona mgonjwa kama wengine walivyomuona bali yeye aliiona IMANI.

Na hapo sasa,imani ikapelekea kupokea uponyaji. Kumbuka hili;
• Imani bila matendo imekufa.
Watu hawa waliomchukua mgonjwa walilijua hili,ndio maana wao pia wakachukua matendo,na imani yao ikathibitika. Maana walipoamini,wakatenda kwa kumchukua mgonjwa na kumpeleka kwa Yesu,ingawa njia ilisonga.
* Unafikirije,kama watu hawa baada ya kuamini wange'kaa na mgonjwa wao peke yao,je mgonjwa huyu ange'ponywa na kusamehewa dhambi zake?

Haleluya....

Yesu Kristo ndio kila kitu,ndani ya vyote.

Ikiwa kama tutafaulu kuishi maisha ya wokovu,maisha ya kumpendeza Mungu Baba,basi nakuhakikishia kabisa,magonjwa yatakuwa si sehemu yetu,wala mavamizi ya mapepo si sehemu yetu.

Maana shetani hana nafasi ndani ya mtu mwenye kumuishia Mungu. Huyo shetani,Kuja atakuja ila hana uwezo wa kumtikisa mwenye imani akatikisika.
Yaani,shetani na mapepo yake hayana nafasi yoyote ndani ya mtu wa Mungu.
Bali yana nguvu na kufanya kazi ndani ya mtu asiyempendeza Bwana Mungu.

Shida kubwa tunayoiona makanisani siku hizi,ni kwamba watu wamekataa kuishi maisha ya WOKOVU,hivyo ibilisi amepata nafasi ya kuwapepeta kama ngano kwa magonjwa,umaskini,laana,mikosi,N.K

Kundi kubwa la watu hawa ni wale wenye kujitambulisha kwamba wao ni wakristo,wameokoka na wanampenda Yesu Kristo,hali wakichomwa mioyo yao kwa kile wakisemacho maana kiko tofauti ukilinganisha na maisha wanayoishi.

Mpendwa ninapokuambia WOKOVU KWANZA maana yake ni kugeuka moja kwa moja kutoka katika hali ya dhambi,kwa kumuelekea Bwana Yesu Kristo pasipo kuangalia nyuma.
Tena ni kukata shauri kabisa kabisa.

Hajalishi mazingira yanasemaje,iwe unachukiwa au la!
Iwe hata kama ukiokoka na kugeuka kabisa kabisa kwamba utatengwa,au utakosa misaada,nasema hivi potelea mbali bhana !
YESU ATAKUSHINDIA TU.
Maana;
YESU ATOSHA..YEYE ATAREKEBISHA,NA KUKUINUA HAPO ULIPO.

Muda wa kuigiza igiza ndani ya wokovu umekwisha kabisa,ikiwa kama ulikuwa ukiigiza hapo awali,sasa nakuomba UACHE.
Maana ndani ya WOKOVU hakuna maigizo,wala usanii.Na sasa ni kuanza upya,nasema upya kumuelekea Bwana Yesu,kuacha vyote kwa ajili yake Bwana. Hapo sasa utaona Mungu akikupigania kwa kila jambo ulifanyalo.

Ikiwa ni binti;
Usikubali hata mara moja mtu akuchezee usichana wako,wewe ni wa thamani sana. Hata kama ni mchumba wako akuchezeaye kwa kigezo cha kukuoa ;
Nasema hivi, hakuna uchumba wa kuchezeana.

Au hata kama ukimkatalia kwamba atakuacha,na kukosa kupata misaada kutoka kwake,POTELEA MBALI! USIKUBALI,tena mwache aende zake! maana yupo mtu sahihi aliyeandaliwa na Bwana,Bwana atamleta,Bali huyo mwache aende zake!

*Ili huyo wa Bwana aje;yakupasa kuishi maisha ya WOKOVU KWANZA.

Ikiwa ni mwanaume;
Endelea kutunza utakatifu wako,USIKUBALI kuyafuata matakwa ya mwili kwa kutamani wanawake,au mambo yaliyo nje ya uwezo wako,subiri wakati wa Bwana,ukifika yatakuja yenyewe maana ukidumu ndani ya WOKOVU mengine mazuri yote huja kwa kuvutwa kama sumaku,wokovu ni sumaku ivutayo mema.

MWISHO.

*Siku ya leo nataka niombe na wewe,inawezekana kabisa umeokoka lakini bado kuna dhambi zinazokunga'nga'nia,na unashindwa kuziacha,nataka niombe na wewe.

Au yawezekana upo ugonjwa ukutesao kwa muda,pia nataka niombe na wewe.
Pia hata wewe ambaye unahitaji kumpokea Bwana Yesu leo,nataka niombe na wewe.N.K
Piga namba yangu hii;
0655111149.

UBARIKIWE.

Comments